CCM WAOMBA RADHI KUMPIGA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, kimeomba radhi kwa chama cha waandishi wa habari mkoani humo (MRPC) kutokana na kitendo kilichofanywa na wafuasi wa chama hicho tawala, kwa kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi  na kusema kuwa waliohusika watachukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mara, Christopher Sanya, alisema wanaomba radhi kwa mwandishi huyo, Christopher Maregesi pamoja na kwa waandishi wote wa habari wa Mkoa wa Mara
“Mimi kwa niaba ya chama ninaomba radhi kwa kitendo alichofanyiwa….ninakikemea kwani si cha kiungwana,”alisema Sanya na kuongeza: “Tutafanya uchunguzi na wale watakaobainika kuhusika tutawachukulia hatua.”
Aliongeza: “CCM tunathamini mchango wa waandishi wote kwa ujumla, hivyo kitendo kilichofanywa si cha kiungwana.”
Maregesi alishambuliwa Februari 8 mwaka huu na wafuasi wa CCM mjini Bunda, muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho katika Kata ya Nyasura.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post