MCHIMBAJI WA MADINI AUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI ,WALIKUWA WANAGOMBANIA MWANAMKE NA MWENZAKE HUKO KAHAMA

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala

Mchimbaji wa  madini aina ya dhahabu   aliyejulikana kwa jina la  Emmanuele Chacha(29) ameuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na mwanamme mwenzie katika ugomvi wa kugombea mwanamke katika kijiji cha Kalole kata ya Lunguya wilayani Kahama katika mkoa wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangala  kwa vyombo vya habari tukio  hilo limetokea  Januari 10 mwaka huu saa tano usiku katika kijiji hicho cha Kalole wilayani Kahama.

 Alisema Emmanuel Chacha ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini aina ya dhahabu mkazi  Nyangalata wilayani Kahama mwenyeji wa Tarime mkoani Mara  aliuawa kwa kuchomwa kisu kifuani na mchimbaji mwenzake wa madini  Cosmas Mazigo (23) ambaye ni mkazi wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Kamanda Mangala alikitaja chanzo cha mauaji hayo kuwa ni ugomvi wa kugombea mwanamke  ambay bado hajafahamika kitendo ambacho kilisababisha marehemu kuchomwa kisu kifuani na kusababisha kifo chake papo hapo na  mtuhumiwa anashikiliwa kwa  hatua za kisheria.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post