Ukistaajabu ya Musa.....!!! WANAUME WATATU WA FAMILIA MOJA WAOTA MATITI,WAFANYIWA UPASUAJI


Vijana watatu wa familia moja ya  Felipe Ramirez, wamepata balaa kubwa baada ya kuota matiti yaliyosababisha kuchekwa na vijana wenzao waliokuwa wakiwaona kuwa ni mashoga.

Vijana hao kutoka katika Jamhuri ya Dominica ni  Yeuri (17 ), Gabriel (11) na  Daniu Ramírez  (12),  hata hivyo, kwa sasa wanaishi kwa amani baada ya kufanyiwa upasuaji na kuondolewa matiti hayo. 
 

Baba yao mzazi, Felipe Ramirez alifanya jitihada ya kuomba msaada kupitia televisheni na magazeti ili wanawe wafanyiwe upasuaji kwani walikuwa wakiishi katika mateso kwenye jamii yao. 

Baada ya kuomba msaada, Mkurugenzi wa Hospitali ya  Marcelino Velez Santana nchini humo, Dokta  Pedro Antonio Delgado aliamua kuwalipia gharama za upasuaji ambao ulichukua saa mbili. 

Ramirez, alisema: “Wakati wanaingizwa katika chumba cha upasuaji nilikosa raha kwa kuhofia kama watatoka salama nao waliogopa lakini baada ya kutoka, wote tumefurahi sana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post