Tumefikia pabaya!!! WANANCHI WENYE HASIRA WAUA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MWANZA CLEMENT MABINA BAADA YA MAREHEMU KUFYATUA RISASI KATIKA UGOMVI WA SHAMBA,tunaomba radhi kwa picha moja hapa chini

Clement Mabina enzi za uhai wake
Hili ndilo gari lililobeba mwili wa aliyewahi kuwa mwenyekiti wa ccm mkoa mwanza na diwani wa kisesa ndugu Clement Mabina pamoja na mwili wa mwananchi (kijana) anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na Mabina
Mwili wa mabina baada ya kupigwa na wananchi

Mwenyekiti wa zamani wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kisesa wilayani Magu mkoani humo, ameuawa na wananchi wenye hasira katika ugomvi wa mashamba.
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi Wilayani Magu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu Desdery Kiswaga, tukio hilo limetokea  leo majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha Kanyama wilayani Magu.
Imeelezwa kuwa Mabina alifika katika eneo hilo kwa ajili ya kupanda miti katika milima ya Kanyama eneo ambalo analimiliki na ambalo hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro baina yake na wananchi.
Imeelezwa kuwa chanzo cha kuuawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?
Wananchi walimhoji sababu za kupanda miti katika eneo hilo ambalo bado lina mgogoro wa umiliki na kutokea kutokuelewana, jambo lililomfanya Mabina kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya, huku moja ikimpiga mtoto na kupoteza maisha papohapo.
Taarifa zimeeleza kuwa kutokana na tukio hilo wananchi walimzingira Mabina na kuanza kumpiga kwa silaha mbalimbali za jadi kama mapanga, fimbo, mawe na mikuki na kusababisha kifo chake papo hapo huku Mabina akifyatua risasi na kusababisha kifo cha kijana mmoja hali iliyowafanya wananchi kumpa kipigo Mabina.

Mabina ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, kabla ya kuwa Diwani, alishindwa katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza mwaka jana na Waziri wa zamani na Mbunge wa zamani wa Ilemela Antony Diallo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments