Majanga!!!!JAMAA ACHINJA MKE WAKE KWA PANGA ,BAADA YA MAUAJI ANYWA SUMU,ASHINDWA KUFA HUKO KAHAMA


Mwanamke mmoja aitwaye  Kwezi Seleli (20) ameuawa kwa kuchinjwa na mme wake wakiwa wamelala nyumbani kwa katika kijiji cha Kalama,kata ya Uyogo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tukio hilo limetokea jana saa kumi alfajiri Chalia Samweli (25) mkazi wa kijiji hicho,alimchinja mke wake kwa kutumia panga na baada ya mauaji jamaa akafanya jaribio la kujiua kwa kunywa sumu aina ya Diazone  inayotumika kuogeshea mifugo bila mafanikio.


Jeshi  la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi kuhusu tukio hilo unafanyika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post