Haijawahi kutokea Afrika !!!MABASI YA KUTEMBEA MAJINI NA NCHI KAVU (Amfibus ,Amphibious Bus) KUINGIA TANZANIA 2014,TAZAMA HAPA VIDEO IKIONESHA MABASI HAYO TANGU YAKIWA YANATENGENEZWA HADI MAJARIBIO

Video ya Basi hilo tangU Linatengenezwa hadi Linafanyiwa majaribio majini na nchi kavu

Kampuni ya Transevents Marketing Ltd ya Tanzania kwa kushirikiana na kampuni la Dutch Amfibious Transport(DAT) linalotengeneza mabasi  kutoka Uholanzi  yenye uwezo wa kutembea nchi kavu na majini na ambayo itakuwa ni Teknolojia ya kwanza kwa Afrika itakayoanzia Tanzania.


Mabasi hayo ya aina yake ambayo yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria wa kutosha yanatarajiwa kuzinduliwa mwakani nchini Tanzania , pamoja na hayo mabasi hayo yataweza kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa na kurahisisha sala zima la usafiri ambapo mabasi hayo na baadhi ya magari mengine madogo yatakuwa na uwezo wa kupita majini na Nchi kavu.



Baadhi ya Mabasi hayo yatakuwa yanatokea Mombasa hadi Mtwara kupitia Baharini kisha nchi kavu. Mchakato huu umekwisha anza kufanyiwa upembuzi yakinifu  kwa ushirikiano na taasisi pamoja na Mamlaka mbalimbali za hapa nchini zikiwemo, SUMATRA, Jeshi la Polisi na kitengo cha Usalama barabarani.

Credit-Michuzi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post