 |
Kamera za malunde1.blogspot.com zimenasa tukio la wanyama aina ya punda wakiwa wamebebeshwa mzigo mzito wa mahindi kama unavyoona katika picha leo mjini Shinmyanga .Kubebeshwa mizigo mizito ni miongoni mwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanyama |
 |
sheria za kuzuia na kupambana na ukatili
wa wanyama zipo kama vile sheria namba 154
ya mwaka 2010 ambayo inasema kwamba
mtu yeyote akifanya ukatili dhidi ya mifugo na ndege,mtu huyo anastahili
kifungo cha mwezi mmoja au kulipa faini kiasi cha shilingi laki moja au vyote
viwili
|
 |
Lakini pia mbali na
faini au kufungo hicho kwa wale wanaonyanyasa wanyama ikiwemo kuning’iniza mifugo au ndege miguu
juu kichwa pia kuna faini ya papo
kwa papo ya kiasi cha shilingi elfu hamsini. |
 |
Miongoni mwa vitendo vya kikatili vinavyofanywa na binadamu
dhidi ya wanyama hao kuwa ni kuwabebesha mizigo mizito, kuwafanyisha kazi kwa muda
mrefu bila mapumziko, lakini pia kuwacharanga mapanga pindi wanapoingia kwenye
mashamba ya watu |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment