WAHAMIAJI HARAMU ZAIDI YA 200 WAKAMATWA SHINYANGA,YUMO PIA MCHINA MMOJA

Kushoto  ni afisa uhamiaji mkoa wa Shinyanga Bi Anna maria Yondani akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mapema leo kuhusu utendaji kazi idara ya uhamiaji mkoa Shinyanga ambapo katika kipindi cha kuanzia mwezi Juni hadi tarehe 2 Octoba mwaka huu wamekamata wahamiaji 223 mkoani humo na miongoni mwao kuna wakenya 15,mchina 1,waganda 13,raia wa Demokrasia ya Congo,24,Rwanda 47,Burundi 69,Afrika Kusini 2,Mexico 1 na watanzania 49 waliohisiwa kuwa sio raia wa Tanzania.Kulia ni Afisa uhamiaji Sajenti Edmund Beda Kiwango ndani ya ofisi ya afisa uhamiaji mkoa wa Shinyanga

Waandishi wa habari wakifuatilia taarifa ya utendaji kazi idara ya uhamiaji mkoa wa Shinyanga ambapo kumefanyika doria,misako na oparesheni lengo likwa ni kukamata na kudhibiti wimbi la wahamiaji wasio rasmi

Kushoto ni Stephen Kidoyayi mwandishi wa habari gazeti la Jamboleo akiandika mawili matatu kuhusu taarifa ya afisa uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Mary  Yondani mapema leo ambapo miongoni mwa wahamiaji haramu waliokamatwa wamefikishwa mahakamani na wengine kufukuzwa nchini na wengine wanaendelea kuhojiwa

Waandishi wa habari wakiwa ndani ya ofisi ya afisa uhamiaji mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post