KESI YA KUMKATA MKONO ALBINO YAAHIRISHWA-KAHAMA



Na Ali Lityawi----

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Sam Rumanyika ameahirisha kesi inayowakabili washitakiwa watatu wanaokabiliwa na shitaka la shambulio lililomsababishia ulemavu wa kudumu mlemavu wa ngozi Kabula Nkalango, kutokana na kukosekana wakili wa upande wa washitakiwa.

Katika shauri namba 2/2012 la kosa la jinai lililokuwa likiwakabili washitakiwa Senga Mabirika, Magobo Njige na Bupina Mihayo ambayo ilikuwa imepangwa kusikilizwa juzi kwa mara ya kwanza, Mahakama Kuu iliyofanyika wilayani Kahama iliahirishwa baada ya washitakiwa kuwa na wakili mmoja badala ya kila mmoja kuwa na wake.

Jaji Rumanyika aliamua kuhairisha kesi hiyo baada ya upande wa washitakiwa kuwa na wakili mmoja ambaye ni John Ng’wigulila badala ya kila mshitakiwa kuwa na wakili wake wa utetezi mahakamani hapo.

Washitakiwa wote watatu wanatuhumiwa kwa kosa la kumkata mkono mlemavu wa ngozi, Kabula Nkalango.

Tukio hilo lilitokea katika kijiji cha Luhaga wilayani Bukombe mkoani Shinyanga mwaka 2012.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments