
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga na taifa kwa ujumla limepata msiba kufuatia kifo cha askari polisi Rehema James (30) kufariki dunia papo hapo hapo jana jioni baada
ya kugongwa na gari katika eneo la Kambarage mjini Shinyanga akiwa amepakizwa kwenye baiskeli maarufu daladala hapa mkoani Shinyanga.
Akizungumza na malunde1.blogspot.com, Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amesema askari aliyefariki dunia ni WP 5090, PC Rehema James Mniko.
Amesema askari huyo akiwa amepakizwa kwenye baiskeli maarufu
kama daladala ghafla aligongwa na gari
aina ya scania lenye namba za usajili BLQ 546 na kufariki dunia papo hapo wakati mwendesha baiskeli akijaribu kulipita gari hilo wakati likikata kona .
Amesema tayari
mwili wa marehemu umesafirishwa kwenda nyumbani kwao Kitunda jijini Dar es salaam
kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho jumapili.
Chanzo cha ajali hiyo
bado kinachunguzwa na jeshi la polisi.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU ASKARI REHEMA. AMINA!
Post a Comment