HATIMAYE DK. ULIMBOKA AMTAJA ALIYE HUSIKA NA KUTEKWA KWAKE ...!Dk Stephen Ulimboka
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Stephen Ulimboka leo ameeleza ya moyoni baada ya kutoa taarifa yake kwa vyombo vya habari kupitia kwa wanasheria wake ambao ni Shayo na Nyaroro Kichere. Taarifa hiyo
imeeleza kuwa aliyekuwa anawasiliana nae kabla ya kutekwa, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande usiku wa Juni 26 mwaka huu ni Bwana Ramadhani Ighondu ambaye alidaiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS). Katika taarifa hiyo Dk. Ulimboka anaeleza kushangazwa na kutokamatwa mtu huyo mpaka sasa na kudai kuwa yeye yupo tayari kutoa ushirikiano kwa tume huru japo mpaka sasa haijaundwa.
Chanzo: Kilimanjaro Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post