Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MARIDHIANO SI UDHAIFU,NI UKOMAVU:RAIS SAMIA



Na mwandishi wetu, Zanzibar

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema maridhiano si udhaifu, bali ni ukomavu wa kisiasa unaojenga misingi ya umoja na kuheshimiana.

Amesema maridhiano ni ishara kwamba viongozi wanaweza kutofautiana kwa hoja, lakini wakakubaliana katika mambo ya msingi ya uendeshaji wa nchi, kujali maslahi na ustawi wa wananchi na nchi kwa ujumla.

Rais Samia ameyasema hayo visiwani Zanzibar leo, Alhamisi Julai 9, 2026 alipohutubia wakati wa hafla ya utiaji saini Tamko la Pamoja la Maridhiano ya Kisiasa Zanzibar.

Amesema mwelekeo huo wa kiungwana, unafungua ukurasa mwingine katika kuimarisha umoja, amani, utulivu na mshikamano wa wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

“Hakika jitihada hizi zinahitaji kuendelezwa na kuenziwa. Nimesema jambo hili la kiungwana kwa kuwa uungwana unatufunza siasa za kushindana kwa hekima na sio kupaza sauti bila mantiki,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com