Shule ya Savannah Plains Secondary School (S5472) iliyopo Mjini Shinyanga imeendelea kudhihirisha ubora wake katika taaluma baada ya kufanya vizuri kwenye Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2026 yaliyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA).
Matokeo hayo yanaonesha kuwa kati ya watahiniwa 45 waliosajiliwa, 43 walifanya mtihani huku wawili wakikosa kufanya mtihani. Watahiniwa wote 43 waliomaliza mtihani wamefaulu kwa asilimia 100, hakuna aliyepata Daraja la Tatu, Nne wala Sifuri.
Katika matokeo hayo, wanafunzi 16 wamepata Daraja la Kwanza (Division I) na wanafunzi 27 wamepata Daraja la Pili (Division II), jambo linaloonyesha kiwango cha juu cha ufaulu na maandalizi bora ya wanafunzi hao.
Kwa mujibu wa taarifa za NECTA, shule hiyo imepata GPA ya 2.3798 (Grade C), huku masomo mengi yakionyesha kiwango kizuri cha ufaulu. Aidha, hakuna mwanafunzi aliyefutiwa matokeo wala kushindwa mtihani.
Mafanikio hayo yanaendana na mwenendo wa kitaifa ambapo NECTA imetangaza kuwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Sita 2026 umeongezeka, huku asilimia 99.92 ya watahiniwa wa shule wakifaulu. Idadi ya waliopata Daraja la Kwanza imeongezeka kutoka 61,020 mwaka 2025 hadi 67,606 mwaka 2026, ikiashiria kuimarika kwa kiwango cha elimu nchini.
Uongozi wa Savannah Plains umepongeza wanafunzi, walimu, wazazi na wadau wote wa elimu kwa ushirikiano wao uliochangia mafanikio hayo, ukieleza kuwa matokeo hayo ni matunda ya nidhamu, kujituma na mazingira bora ya kujifunzia.
"Hongera wanafunzi wa Kidato cha Sita 2026. Tunajivunia mafanikio yenu makubwa katika mtihani wa ACSEE. Endeleeni kuwa mabalozi bora wa Savannah Plains na Taifa kwa ujumla."

Social Plugin