Mradi wa Nickeli wa Kabanga ambao ni miongoni mwa uwekezaji mkubwa wa kimkakati wa madini na viwanda nchini Tanzania, umekaribia kuanza utekelezaji wake hatua ambayo imefikiwa kufuatia kikao cha MRADI WA KABANGA NICKEL MBIONI KUANZA
ya juu cha kutoa taarifa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu hatua iliyofikiwa katika majadiliano yanayoendelea na maandalizi ya mradi huo.
Taarifa hiyo iliyowasilishwa Ikulu na Bw. Keith Liddell, Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Kabanga Nickel Limited na Lifezone Metals (NYSE: LZM), kwa kushirikiana na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, viongozi wote wawili walisisitiza tena nia yao ya kuuendeleza mradi huo kwa namna ambayo italeta faida kubwa zaidi kwa Tanzania.
"Ilikuwa heshima kubwa sana kukutana na Mhe. Rais, amesisitiza tena nia yake thabiti kwenye mradi huu na msaada wake katika kuuendeleza mradi huu chini ya mpango wa utekelezaji uliokubaliwa," alisema Bw. Liddell
Kwa upande wake Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu aliuweka mradi wa Kabanga kama mradi wa mabadiliko makubwa na wenye uwezo wa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa viwanda nchini Tanzania, utengenezaji wa fursa mpya za ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.
Alisema lengo la Serikali siku zote limekuwa ni kuhakikisha kuwa uchenjuaji wa madini unafanyika nchini Tanzania ili nchi ipate faida kubwa zaidi kutoka kwenye rasilimali zake za madini, akikiri kwamba majadiliano ya mradi mkubwa kama huu ni mgumu na yanachukua muda, lakini alisema mazungumzo ya hivi karibuni yamesaidia kutatua masuala kadhaa yaliyokuwa bado hayajakamilika na yameleta njia nzuri ya kusonga mbele kwa maslahi ya pande zote mbili.
Bwana Mchechu alibainisha kuwa mradi huo unatarajiwa kuleta faida kubwa kupitia ushiriki wa wazawa (local content), kodi, gawio, uhamishaji wa teknolojia na maendeleo ya viwanda, akisema mradi huu unaobadilisha mwelekeo, pamoja na uwekezaji mwingine wa kimkakati, una uwezo wa kuharakisha mabadiliko ya viwanda nchini Tanzania na malengo ya maendeleo ya muda mrefu.
Mradi wa Kabanga Nickel unatarajiwa kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji mkuu katika mnyororo wa usambazaji wa madini muhimu duniani, huku ukihakikisha uongezaji mkubwa wa thamani unafanyika hapa nchini.

Social Plugin