Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya la Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga (PCCB House Shinyanga)
Mkurugenzi wa Milki wa TAKUKURU, Dkt. Emmanuel Kiyabo, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo jipya la PCCB House Shinyanga, akieleza hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo pamoja na miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa TAKUKURU.
Na Kadama Malunde, Shinyanga
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuonesha dhamira ya dhati ya kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini kupitia uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambapo leo imezinduliwa rasmi Ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga iliyopo katika mtaa wa Miti Mirefu 'Uzunguni' Mjini Shinyanga iliyojengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.6.
Uzinduzi huo umefanywa na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, huku ukihudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, mila pamoja na wananchi mbalimbali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Chalamila amesema Serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika TAKUKURU kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini.
Amesema TAKUKURU kwa sasa ina ofisi 145 nchini zikiwemo ofisi za mikoa, wilaya na vituo maalum, huku majengo 70 pekee yakiwa yanamilikiwa na taasisi hiyo. Aidha, majengo mengine 11 yanaendelea kujengwa katika mwaka wa fedha 2025/2026.
“Kwa idadi hii ya majengo ya ofisi za TAKUKURU, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa unaodhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mapambano dhidi ya rushwa nchini,” amesema Chalamila.
Ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha TAKUKURU kupitia rasilimali watu, vitendea kazi na fedha zinazowezesha utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa Chalamila, jengo hilo limejengwa kwa gharama ya Shilingi 1,602,048,068.92 na ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuhakikisha ofisi za TAKUKURU nchini zinakuwa na makazi ya kudumu yanayokidhi mahitaji ya utendaji kazi wa kisasa.
Aidha, amewataka watumishi wa TAKUKURU kuyatunza majengo na vifaa vinavyotolewa na Serikali ili viweze kuendelea kutoa huduma kwa muda mrefu na kuleta tija iliyokusudiwa.
Katika hafla hiyo, Chalamila pia ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na TAKUKURU kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhakikisha fedha za umma zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila (kushoto), akifungua rasmi jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga.
Amesisitiza kuwa uwazi, uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika kusimamia miradi ya maendeleo ni nyenzo muhimu katika kuziba mianya ya rushwa na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana katika miradi inayotekelezwa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mohamed Mhita, amesema jengo hilo ni uwekezaji muhimu utakaoongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa katika Mkoa wa Shinyanga.
Amesisitiza kuwa vita dhidi ya rushwa vinahitaji ushiriki wa kila mwananchi na si jukumu la TAKUKURU pekee.
“Uwekezaji huu utaongeza kasi ya kupambana na rushwa katika Mkoa wa Shinyanga. Vita dhidi ya rushwa vinahitaji ushiriki wa kila mmoja wetu. Tujenge utamaduni wa kupinga rushwa kwa vitendo katika jamii zetu,” amesema Mtatiro.
Ameongeza kuwa jengo hilo linapaswa kuwa kitovu cha haki, uwajibikaji na uadilifu kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani.
Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Erenestina Richard, aliyemwakilisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, ameipongeza TAKUKURU kwa juhudi zake katika mapambano dhidi ya rushwa na kuomba taasisi hiyo kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu kwa wananchi wa vijijini.
Amesema wananchi wengi wa maeneo ya vijijini bado wanahitaji elimu zaidi kuhusu madhara ya rushwa na namna ya kushiriki katika kuzuia na kupambana na vitendo hivyo.
“Tunaiomba TAKUKURU kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wa vijijini ili waweze kuelewa madhara ya rushwa na wajibu wao katika kuzuia vitendo hivyo,” amesema.
Awali akiwasilisha taarifa ya mradi, Mkurugenzi wa Milki wa TAKUKURU, Dkt. Emmanuel Kiyabo, amesema ujenzi wa jengo hilo ulitekelezwa kwa kipindi cha miezi 10 kwa gharama ya Shilingi bilioni 1.6.
Ameeleza kuwa mradi huo umehusisha ujenzi wa jengo la kisasa lenye ghorofa moja pamoja na miundombinu mingine muhimu na samani za kisasa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa TAKUKURU.
Dkt. Kiyabo amesema matumizi ya mfumo wa “Design and Build” uliowashirikisha wataalamu kutoka TAKUKURU na Jeshi la Magereza yamesaidia kupunguza gharama za ujenzi na kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa mradi huo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo akiwemo Chifu Kidola Njange wamesema Uzinduzi wa jengo hilo ni hatua muhimu katika kuimarisha uwezo wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi, sambamba na kuunga mkono jitihada za Serikali za kujenga Tanzania yenye uwajibikaji, uadilifu na maendeleo endelevu.
TAZAMA PICHA ZAIDI HAPA CHINI
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga.

Muonekano wa sehemu ya jengo la kisasa la PCCB House Shinyanga lililozinduliwa rasmi Juni 4, 2026, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Muonekano wa sehemu ya jengo la kisasa la PCCB House Shinyanga lililozinduliwa rasmi Juni 4, 2026, ikiwa ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo jipya la Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga (PCCB House Shinyanga)
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akikagua jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wake rasmi.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila (kushoto), akifungua rasmi jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jijini Shinyanga. Kulia ni kuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mohamed Mhita.
Mkurugenzi wa Milki wa TAKUKURU, Dkt. Emmanuel Kiyabo, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo jipya la PCCB House Shinyanga, akieleza hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo pamoja na miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa TAKUKURU.

Mkurugenzi wa Milki wa TAKUKURU, Dkt. Emmanuel Kiyabo, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo jipya la PCCB House Shinyanga, akieleza hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo pamoja na miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa TAKUKURU.
Mkurugenzi wa Milki wa TAKUKURU, Dkt. Emmanuel Kiyabo, akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa jengo jipya la PCCB House Shinyanga, akieleza hatua mbalimbali za utekelezaji wa mradi huo pamoja na miundombinu iliyojengwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa TAKUKURU.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini, Erenestina Richard, akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Francis Chalamila, akipanda mti wa kumbukumbu kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, akipanda mti wa kumbukumbu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga.
Picha za pamoja
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Social Plugin