Na mwandishi wetu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi amewahakikishia Watanzania kuwepo na Amani na Usalama ambapo pia amesema wizara yake itakua wizara muhimu itakayosaidia taifa kupata maendeleo endelevu na kutenda haki kwa wananchi wote.
Waziri Katambi ameyasema hayo wakati wa Hafla ya Kugawa Tuzo na Vyeti kwa watumishi raia askari na watumishi raia ambao wamefanya vizuri katika mwaka wa fedha 2025/2026 ambayo ilihudhuriwa pia na Naibu Waziri,Ayoub Mohammed Mahmoud,Katibu Mkuu,Ally Senga Gugu,Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Maduhu Kazi,Wakuu wa Vyombo vya Usalama vilivyopo chini ya wizara,Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama,Najma Murtaza Giga,Viongozi wa Dini,Viongozi na Wananchi kutoka Majimbo ya Shinyanga Mjini,Chaani Zanzibar.
“Ni matatajio ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuona nchi yetu inabaki kuwa na uzalendo,utaifa na mshikamano wa Muungano wetu,hivyo basi hatuna budi kwa Wafanyakazi wote wa umma wanaofanya vizuri kuwapongeza na kutambua mchango wao kwa kile wanachofanya”amesema Waziri Katambi.

Social Plugin