Mwigizaji mkongwe wa tasnia ya filamu nchini (Bongo Movie), Hashim Kambi, amefariki dunia leo Aprili 27,2026 Jijini Dar es salaam.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mwigizaji mwenzake, William Mtitu, ambaye ameeleza kwa masikitiko makubwa kuhusu msiba huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwigizaji mkongwe wa filamu nchini, Hashim Kambi kilichotokea leo, Dar es Salaam. Taifa limepoteza kipaji adhimu kilichochangia kwa kiasi kikubwa kukuza na kuitangaza tasnia ya filamu nchini.
Ninatoa pole kwa Shirikisho la Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wasanii wa filamu nchini, familia ya marehemu, wadau wa filamu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un." - Rais Samia Suluhu Hassan



Social Plugin