Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BALOZI MATINYI AFUTURU NA DIASPORA WA SWEDEN NA KUWAAGA

Balozi Mobhare Matinyi, ametoa nasaha za kipekee na kuwaaga Watanzania waishio nchini Sweden wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania jijini Stockholm. 

Tukio hilo lililoshirikisha Watanzania mbalimbali wakiwemo wanafunzi, wafanyabiashara na familia za Watanzania, limefanyika katika ukumbi wa Ubalozi huku akionyesha mshikamano na umoja wa Watanzania.

Balozi Matinyi amewashukuru Watanzania kwa juhudi zao za kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden. 

Akisisitiza umuhimu wa kudumisha maadili ya Umoja, Amani na Mshikamano hasa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, Balozi Matinyi amesema ni Muhimu kujenga na kuimalisha umoja na mashikamano baina yao. 

Ameelezea furaha yake kwa kuona Watanzania wakikusanyika kwa pamoja, katika mfungo wa Iftar, na kuonyesha mfano wa mshikamano na upendo kati ya taifa lao na jamii nyingine zinazowazunguka amesema ni wakati wa kutafakari na kujenga imani ya Watanzania. 

"Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, ni wakati wa kutafakari na kujenga imani yetu, lakini pia ni wakati wa kutenda mema kwa wenzetu na kujali zaidi maslahi ya jamii yetu ya Tanzania hapa nchini Sweden," amesema Balozi Matinyi. 

Amewakumbusha pia Watanzania hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa nchi yao na kutoa mchango wao katika shughuli za kijamii na kiuchumi katika mazingira ya kimataifa.

Aidha, Balozi Matinyi amewataka watanzania hao kutoa ushirikiano mkubwa kwa viongozi mbalimbali kutoka nchini Tanzania wanaoletwa na serikali kuhudumu ili kuleta maendeleo, umoja na mshikamano.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com