Mwezeshaji wa Mafunzo ya Kupambana na Habari Potoshi (Fake News), Misinformation na Disinformation, Kadama Malunde – Mkurugenzi wa Malunde 1 Blog akifundisha mbinu za uthibitishaji wa taarifa (fact-checking), matumizi ya Akili Unde (AI) katika kuhakiki habari, pamoja na namna ya kutambua asili ya picha na video.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Fact Checking, Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Malunde 1 Blog, akieleza mbinu za kutambua na kupambana na taarifa potofu kwa waandishi wa habari mkoa wa Tabora
Mwezeshaji wa Mafunzo ya Uthibitishaji na Uhakiki wa Taarifa Kadama Malunde kutoka Malunde Media akifundisha mbinu za kupambana na taarifa potofu, upotoshaji wa taarifa pamoja na habari za uongo kwa waandishi wa habari Mkoa wa KageraKatika ulimwengu wa habari za kidijitali, ambapo uzushi (Fake News) na Akili Unde (AI) vinaweza kupotosha ukweli kwa sekunde, tunahitaji mashujaa wenye darubini kali. Kutana na Kadama Malunde, mwanahabari nguli na mdau wa @tanzaniabloggersnetwork (TBN) anayepambana mchana na usiku kuhakikisha habari unayosoma ni ya kweli!
Kama mwanzilishi wa Malunde 1 Blog (Malunde.com), Kadama amekuwa sauti ya Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla. Lakini mwaka huu, amevaa joho la ualimu kuokoa tasnia ya habari. 🎓✨
Nini kipya?
Malunde amekuwa akizunguka nchini akifundisha wanahabari mbinu za kisasa za Uhakiki na Uthibitishaji wa Taarifa (Fact-Checking). Hadi sasa:
📍 Ameshafika mikoa ya Tabora, Geita, na Kagera.
👥 Amewanoa zaidi ya wanahabari 60+ kuwa walinzi wa ukweli.
🤖 Anawafundisha waandishi wa habari jinsi ya kubaini picha na video za kugushi za AI ili wasingie kwenye mtego wa 'matango pori'.
"Nafurahia kutoa ujuzi huu kila ninapofundisha," anasema Malunde, akiamini kuwa mwandishi aliye tayari kuthibitisha na kuhakiki taarifa ni muhimili wa amani na mshikamano wa Taifa letu. 🇹🇿
TBN inajivunia kuwa na watu wenye weledi kama Kadama Malunde, wanaoambukiza wengine ujuzi ili kuifanya tasnia ya habari kuwa "Eneo Salama."
#KadamaMalunde #Malunde1Blog #TBN #UhakikiWaHabari #FactChecking #Tanzania #HabariZaUkweli #DigitalJournalism #SayNoToFakeNews #Uzalendo
soma pia



Social Plugin