Na Hadija Bagasha Mkinga,
Mgombea Ubunge jimbo la Mkinga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Twaha Mwakioja amechukua fomu Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi (INEC) yakuomba kuteuliwa nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Baada ya kukabidhiwa fomu Mwakioja amekishukuru chama chake chini ya Mwenyekiti Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo.
Akizungumza nje ya ofisi ya msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mkinga baada ya kuchukua fomu mgombea ubunge wa Jimbo la Mkinga kwa tiketi ya chama cha mapinduzi ccm, Twaha Mwakioja hapa anaelezea vipaumbele ambavyo wananchi wa jimbo hilo watakakwenda kunufaika navyo ikiwemo kuboresha sekta hiyo ya uvuvi lakini pia ameahidi kuharakisha maendeleo ya wanamkinga katika Nyanja mbalimbali
"Ikiwa tume itaniteuwa kugombea nafasi hii naahidi kufanya kampeni za kiustaarabu zenye kujali utu na hatimae kupata kura nyingi za Urais,ubunge na udiwani nina imani tutapata ushindi wa kishindo.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya Wananchi Wilayani Mkinga Mkoani Tanga wamesema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa zana za uvuvi ikiwemo nyavu zinazokidhi viwango kwajili ya kuvulia samaki hatua ambayo imewasababishia kushindwa kupata mazao bora baharini ambapo wamemuomba Mbunge ajaye kwenda kusukuma sekta hiyo ambayo ndio kitega uchumi pekee wanachokitegemea kuendeshea maisha yao.
Wananchi hao wamesema kuwa, mwanaCCM aliyepitishwa kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Mkinga Twaha Mwakioja wanaamini ataweza kuwasaidia kutatua changamoto hiyo ambayo inakwenda kufungua uchumi wa Mkinga na kuchochea ajira kwa vijana.
Aidha wananchi hao wamesema licha ya changamoto hiyo katika sekta ya uvuvi lakini pia wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya elimu,afya na uchumi ambazo wanatamani kuona mbunge ajae anaweza kuanza kuzitatua ili kuweza kuleta maendeleo yao.







Social Plugin