
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa nafasi ya Ubunge na Uwakilishi wa Viti Maalum kundi la Vijana, Ndg. Mohammed Abood Mohammed ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ametangaza matokeo rasmi ya mchakato.
Uchaguzi huo umefanyika tarehe 01 Agosti 2025 katika Ukumbi wa Jiji uliopo Mtumba, Dodoma na Mkurugenzi wa Uchaguzi alikuwa ni Katibu Mkuu wa UVCCM, Ndg. Jokate Urban Mwegelo na matokeo yapo hivi:
Tanzania Bara wagombea 31 ambapo kati yao zinatakiwa nafasi sita (6)- kura zilizopigwa 2,466 zilizoharibika 12 na kura halali ni 2,454.
1. Ng’wasi Damas Kaman - 409
2. Jesca John Magufuli - 391
3. Halima Abdallah Bulembo - 320
4. Lulu Guyo Mwacha - 316
5. Juliana Didas Masaburi - 282
6. Timida Mpoki Fyandomo - 280
Zanzibar wagombea walikuwa 17 na nafasi ni nne (4) - kura zilizopigwa 1,652 zilizoharibika 8 na kura halali 1,647.
1. Mwanaenzi Hassan Suluhu - 399
2. Latifa Khamis Juakali - 357
3. Zainab Abdallah Issa - 334
4. Amina Ali Mzee - 151
Nafasi ya Uwakilishi katika Baraza la Wawakilishi wagombea walikuwa 10 na nafasi ni mbili - kura zilizopigwa 822 zilizoharibika 04 na kura halali 818.
1. Salha Muhammed Mwinjuma - 255
2. Hudhaina Mubarak Tahir - 233
Social Plugin