Na Hadija Bagasha - Tanga
Mgombea Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mujaheed Mkadamu, leo tarehe 27 Agosti 2025 amerudisha rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Milingano, iliyopo Wilaya ya Muheza, Mkoa wa Tanga.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu hiyo, Mkadamu ameahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kata hiyo, akitaja kwa kipaumbele tatizo sugu la upatikanaji wa maji safi na salama.
Aidha, amesisitiza kuwa endapo atachaguliwa, atahakikisha anashirikiana na wananchi na viongozi wa serikali kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hiyo pamoja na kuboresha huduma nyingine za kijamii kama elimu, afya na miundombinu.
Mkadamu pia amewashukuru wananchi kwa moyo wa ushirikiano na kuwataka kuendelea kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi.






















Social Plugin