MALKIA WA NGUVU JENIFA ALPHAYO ATAKA WANAWAKE KUFANYA KAZI KWA BIDII


Na Woinde Shizza ARUSHA

Wanawake wametakiwa kutokukata tamaa katika kazi zao pamoja na kufanya kazi kwa nguvu na bidii huku wakimtegemea Mungu ili waweze kuondokana na umaskini.


Hayo yameelezwa na Malkia wa Nguvu Jenifa Alphayo mshindi wa nafasi ya The Best Designer of the Year Afrika Wear alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo za wanawake wajasiriamali iliyoandaliwa na kampuni ya phide intatament ambapo alisema kuwa niwakati sasa wa wanawake kuamka na kuanza kuchapa kazi.


Aliwataka wanawake kutokata tamaa katika kazi zao na wamtegemee Mungu zaidi huku wakichapa kazi Kwa bidii zaidi na sio kwenda kukesha makanisani na kusema wanapokea miujiza kwani hakuna miujiza unaokuja bila ya kujituma na kufanya kazi.


"Kufanya kazi kwa moyo na kupenda kazi unayoifanya ukishapenda kazi unayoifanya utafanyakazi Kwa moyo na kupenda kazi unayoifanya ,mimi mwenyewe nimeanzia chini adi nilipofikia apa nilipo ,Siri ya mafanikio yangu nikupenda kile ninachokifanya", alisema Jenifa.


Aidha alisema kuwa watanzania wengi wamekuwa na tatizo la kutokujali mda kitu ambacho kimewafanya waendelee kubaki katika umaskini hivyo aliwataka wabadilike Ili waweze kutoka kwenye umaskini.


"Waafrika wengi atujali mda ,muda ni fedha ukijali mda lazima ufanikiwe ,ukijali muda lazima ufanikiwe lakini pia unatakiwa ujali wateja ili ufanikiwa ata wakikuuliza maswali ya kijinga wavumilie wajibu vizuri ili wakuuingishe na waweze kurudi tena ,mimi ndio nilichofanya adi kufikia hapa"alisema Jenifa
Jenifa Alphayo mshindi wa nafasi ya mwanamitindo Bora wa nguo za kiafrika (the best designer of the year afrika wear) katika tuzo za wanawake wajasiriamali zilizoandaliwa na kampuni ya phide intatament akishangilia mara baada ya kupokea tuzo hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم