TANGA UWASA YAENDELEA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI



Mhandisi Salum Ngudy akizungumza jambo na wadau wa Maji kuhusiana na miradi ya kuiboresha huduma ya maji safi jijini Tanga
Mitambo ya kusafirisha Maji kutoka Bwawa la mabayani


Na Salma Amour - Tanga

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi Mazingira Tanga (UWASA) katika wiki ya maji inaendelea kutekeleza miradi muhimu ili kuweza kuzalisha maji ya kutosha na wananchi waweze kupata huduma hiyo kwa muda wa saa 24 kama ilivyokuwa hapo awali ambapo hali hiyo imewaathiri wakazi katika maeneo mbalimbali kutokana na mvua kutokunyesha kwa kipindi kirefu na kusababisha maji kupungu katika bwawa la maji.


Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea bwala la Maji huko Pande Mabayani pamoja na mtambo wa kuzalisha Maji Mowe mhandishi wa mamlaka ya Maji Tanga UWASA Salum Ngudy alisema wanaendelea kuboresha huduma ya maji katika jamii.


Awali akiwa katika mitambo wa kutibu Maji mhandisi salum alieleza kuwa Maji yanayotoka kwenye Bwawa kuelekea kwenye mitambo yanasafishwa kila baada ya masaa mawili wanapimwa ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza kuwaathiri wananchi kupitia Maji hayo kwa kuwa wataalamu wa maabara wapo makini katika kuhakikisha maji yanakuwa safi na salama muda wote.



Katika hatua nyingine upatikanaji wa Maji kwa siku katika maeneo yote ni lita 30,000 ambayo katika baadhi ya maeneo Maji hayatoki ingawa kwa sasa mtambo uliopo ni kwa ajili ya kutanua uzalishaji ili kufikia Lita 45,000 ambayo itasaidia kukidhi haja za wananchi wote.


"Tuna mitambo minne ambayo miwili ndiyo inatumika kwa sasa inasaidia kupandisha maji mpaka kuwafikia wananchi na mingine miliwi ipo kwa ajili ya akiba kama ikitokea mmoja kati ya hii ikiharibika", alisema


Awali mhandisi Salum aliwashauri wakazi wa Tanga kupanda miti itakayosaidia kutunza mazingira muda wote na kusababisha kunyesha mvua za mara kwa mara ili kuwepo na upatikanaji wa maji.


"Suala la miti kuwa michache katika maeneo yetu tunayoishi ni changamoto niwaombe wananchi kupanda miti ili kusaidia mazingira yetu muimarika na hata mvua ziweze kunyesha ili tupate maji muda wote",aliongeza.


Aliongeza kuwa kumekuwepo na changamoto ya ukosefu wa Maji Tangu mwezi Novemba Mwaka jana lakini mpaka kufikia Machi mwaka huu hali hiyo imeweza kuimarika hivyo amewaomba wakazi wote kutumia maji kwa umakini na kuweza kuyahifadhi kwenye vyombo mbalimbali itakayo wasaidia katika matumizi yao binafsi.


"Kuanzia Machi Mwaka huu hali ya upatikanaji wa maji imeanza kuwa shwari ingawaje haijafikia asilimia 100 , maeneo mengi yanapata maji kwa takribani saa 20 na vilevile Tanga UWASA tumejipanga kutatua changamoto iliyokuwepo",alisema mhandisi Salum.


Aidha mtaalamu wa maabara kutokea kwenye mtambo wa kutibu Maji Amos Rwehangana alibainisha kuwa kwa sasa hali ya kutoka kwa maji ipo shwari katika maeneo mbalimbali yakiwa masafi na hayawezi kuleta athari yeyote katika jamii hii ni kutokana na juhudi walizonazo.


"Wananchi wetu wanapata huduma ya maji Safi na hii ni kutokana na kuyatibu maji haya ambayo chanzo chake ni kwenye mito ikiwemo mto zigi na huwezi kuyatumia hivyo hivyo bila huyatibu hivyo sisi watu wa maabara tunayafanyia vipimo kila baada ya saa mwili, tunayatia dawa na pia zipo dawa za aina nne tofauti tofauti na haijawahi kutokea wananchi kupata maji yenye madhara kwa kuwa tunaujua wajibu wetu,hivyo kutaendelea kupambana ili wananchi wapate huduma bora kwa matumizi yao",alisema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments