UWT ITWANGI WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI...MBUNGE SANTIEL ASHANGAA WANAUME WANAOBAKA WATOTO

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Santiel Kirumba akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani katika Kijiji cha Kidanda Kata ya Itwangi.

Na Shinyanga Press Club Blog

Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT)Kata ya Itwangi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto ikiwemo kulawiti na ubakaji pamoja na vipigo kwa wakina mama.

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi Mosi,2023 katika Kijiji cha Kidanda Kata ya Itwangi Halmashauri ya Shinyanga ikiwa ni katika kuelekea siku ya kilele March 8,ambapo wanawake wameiomba serikali kuchukuwa hatua kali kwa watu watakaobainika kufanya vitendo vya kulawiti watoto na ubakaji kutokana na kuwa kinyume na maandiko ya dini na sheria ya nchi.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi Mbunge wa Viti maalum (CCM)Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amesema kuna vitendo vya ukatili vinafanyika katika jamii lakini wanawake wengi wanashindwa kutoa taarifa na kusababisha matukio hayo kuendelea.

Kirumba ameitaka jamii kuvunja ukimya na kuwataja watu wanaofanya vitendo hivyo hatua ambayo itasaidia kukomesha ukatili na kuwawezesha watoto wa kike na wa kiume kuwa katika mazingira salama badala ya kuendelea kufumbia macho kwa kuwalinda wahusika.

Katika hatua nyingine Mbunge Kirumba amesikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wanaume kwenye familia kuwalawiti watoto wao na wengine kuwabaka wakati kuna wanawake wengi wa umri wao ambao wanaweza kuzungumza nao na kuwaomba watanzania kulaani vikali vitendo hivyo.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala amewataka wanaume kuacha mfumo dume kwenye familia badala yake washirikiane na wenzi wao ili kuleta maendeleo kwani ubabe hauna tija matokeo yake inakuwa chanzo cha ukatili ndani ya familia na kusababisha kutengana.

Amesema wanawake wengi hawashiriki vikao vya maamuzi ngazi ya Vijiji vinapoitishwa kutokana na waume zao kuwazuia kitendo kinawanyima haki ya kupata taarifa na kujua kinachoendelea pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili ikiwemo huduma za afya,maji na miundombinu ya barabara.
Diwani wa Kata ya Itwangi Sonya Jilala akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika Kijiji cha Kidanda
Mkaguzi wa polisi Kata ya Itwangi Analyze Kaika akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wananchi wa Kijiji cha Kidanda Kata ya Itwangi wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Magreth Mela Katibu wa UWT Kata ya Itwangi akisoma risala kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Santiel Kirumba
Mkaguzi wa polisi Kata ya Itwangi Analyze Kaika akitoa elimu ya ukatili wa kijinsia
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho
Baadhi ya viongozi na madiwani wakiwa kwenye maadhimisho
Maadhimisho yakiendelea

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments