RAFIKI-SDO YAKUTANISHA BARAZA LA WATOTO HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA NA WATOA MAAMUZI KUWASILISHA CHANGAMOTO ZA WATOTO

Meneja wa Shirika la Rafiki- SDO Asante Nselu, (kushoto) akiwa na Meneja mradi wa (MKUA) Tangi Clement (katikati) na Mratibu wa Mradi (TUWALEE) Maria Maduhu kwenye kikao hicho cha viongozi wa Baraza la watoto wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

SHIRIKA la Rafiki-SDO limekutanisha baraza la watoto ngazi ya Halmashauri ya wilayani Shinyanga, pamoja watoa maamuzi wa Halmashauri hiyo, ili kusikiliza changamoto zinazo wakabili watoto na kuzitafutia ufumbuzi.

Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 14,2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, kwa ufadhili wa Shirika la Save the Children na mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT-Trust) na kuratibiwa na Shirika la Rafiki-SDO kupitia mradi wa TUWALEE na MKUA.

Meneja Mradi wa Uimarishaji wa Mabaraza ya watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki-SDO Tangi Clement, amesema mara baada ya kumaliza kuunda Mabaraza ya watoto katika vijiji 51 na kuunda madawati 71, Shule ya Msingi 58 na Sekondari 13, watoto hao waliomba kufanya kikao na watoa maamuzi ngazi ya halmashauri ili kuwasilisha changamoto zinazowakabili watoto na kutafutiwa ufumbuzi.

"Kikao hiki cha leo cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri wilayani Shinyanga walikiomba wenyewe watoto, ili wakutane na watoa maamuzi na kuwasilisha changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watoto na kutafutiwa ufumbuzi," amesema Tangi.

Naye Mratibu wa Mradi wa TUWALEE Maria Maduhu, amewataka watoto kupitia Mabaraza yao, wapaze sauti juu ya masuala ambayo ni kero kwao, vikiwamo na vitendo vya ukatili ambavyo hufanyiwa, ili wasaidiwe na kujengewa mazingira rafiki ya kusoma pamoja na kuimalishiwa ulinzi na usalama.

Nao Viongozi wa Baraza hilo la watoto ngazi ya vijiji, waliwasilisha changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili watoto katika maeneo yao ikiwamo ya upungufu wa madawati, vitabu, matundu ya choo, walimu wa Sayansi, Maabara za sayansi hazijakamilika, ukosefu wa chakula shuleni.

Wametaja changamoto zingine watoto kunyimwa haki yao ya kielimu,kwa kuzuiwa na wazazi kwenda shule ili wakachunge mifugo na kwenda kulima huku wakitoa na mapendekezo mengine kuwa watoto washirikishwe kwenye uandaaji wa Bajeti za Halmashauri na kutoa vipaumbele vyao.

Wametaja mapendekezo mengine, ni kutengewa Bajeti kwa ajili ya kushiriki kwenye maadhimisho ya siku ya watoto, ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, ili wapate fursa ya kushiriki na kupaza sauti juu ya changamoto ambazo zinawakabili watoto.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, amesema changamoto ambazo wameziwasilisha watoto hao, zingine tayari zipo kwenye utekelezaji na zingine watazifanyia kazi.

Aidha, amesema masuala mengine ya watoto ambayo yamewasilishwa yataingizwa kwenye mwaka wa fedha ujao ikiwamo na Bajeti ya Maadhimisho ya siku ya watoto.

Naye Meneja wa Shirika la Rafiki- SDO Asante Nselu, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau, katika masuala mazima ya kutetea haki zao na kutatua baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili ikiwano na utengaji wa bajeti za watoto.

Meneja wa Shirika la Rafiki- SDO Asante Nselu, akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la watoto ngazi ya Halmashauri wilaya ya Shinyanga na watoa maamuzi wa Halmashauri hiyo.

Meneja Mradi wa Uimarishaji wa Mabaraza ya watoto (MKUA) kutoka Shirika la Rafiki-SDO Tangi Clement, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwenye kikao hicho.

Diwani wa Kata ya Ilola wilayani Shinyanga Amos Mshandete akizungumza kwenye kikao hicho cha viongozi wa Baraza la watoto.

Diwani wa Kata ya Usule Ezekiel Seleli akizungumza kwenye kikao hicho cha Viongozi wa Baraza la watoto na watoa maamuzi ngazi ya Halmashauri.

Afisa Elimu ya watu wazima na mfumo usio Rasmi wilayani Shinyanga Christopher Maingu akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Happines Misael akizungumza kwenye kikao hicho.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Killian Mlalama akizungumza kwenye kikao hicho.

Viongozi wa Baraza la watoto ngazi ya vijiji wakiwasilisha changamoto ambazo zinawakabili watoto katika maeneo yao na mazingira ya shule kwa watoa maamuzi wa Halmashauri ili zitafutiwe ufumbuzi.

Uwasilishaji wa changamoto ambazo zinawakabili wa watoto ukiendelea.

Meneja wa Shirika la Rafiki- SDO Asante Nselu, (kushoto) akiwa na Meneja mradi wa (MKUA) Tangi Clement (katikati) na Mratibu wa Mradi (TUWALEE) Maria Maduhu kwenye kikao hicho.

Viongozi wa Mabaraza ya watoto ngazi ya vijiji wilayani Shinyanga wakiwa kwenye kikao chao na watoa maamuzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kuwasilisha Changamoto za watoto ambazo zinawakabili na kutafutiwa ufumbuzi.

Walezi wa Mabaraza ya watoto wakiwa kwenye kikao hicho.

Picha ya pamoja ikipigwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments