WADAU WATAKA KITABU CHA SAMIA KUTAFSIRIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.


Na Dotto Kwilasa,DODOMA

BAADA ya uzinduzi wa kitabu cha Rais Samia Suluhu Hassan,baadhi ya wadau wa lugha ya kiswahili wameshauri kitabu hicho kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili ili kuyafikia makundi yote.

Hatua hiyo imekuja baada ya kitabu hicho kilichopewa jina la "Continuity with Vision the Roadmap to Success for President Samia Suluhu Hassan"kuzinduliwa juzi jijini Dodoma na waziri wa elimu,Sayansi na Teknolojia Prf.Adolf Mkenda kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa . 

Mmoja wa wadau hao Hosea Steven ameeleza kuwa umuhimu wa kitabu hicho utazingatiwa  endapo kitayafikia makundi yote yakiwemo yale ya pembezoni.

"Tunafahamu kuwa kitabu hiki ni muhimu hasa katika maendeleo ya uchumi wa nchi yetu,tunategemea kuona Kila mwananchi anasapoti kazi za Rais wetu Kupitia hiki kitabu na ili kufikia malengo hayo lazima pia kiandikwe kwa lugha ya wengi,"amesisitiza .

Naye mmoja wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha mipango na maendeleo vijijini Ayub Makali amesema kitabu cha Continuity with Vision the Roadmap to Success for President Samia Suluhu Hassan kinakwenda kujibu maswali ya Watu wengi na makundi mbalimbali kuhusu hoja nyingi zilizomo kwenye jamii.

Amesema  kitabu hicho kimetumia muda mchache kuandikwa kutokana na ukweli kwamba Rais wa awamu ya Sita amekuwa Mtendaji kwani kwa Kipindi kifupi ameweza kufanya mengi.

Awali akiongea katika Uzinduzi huo mkuu wa chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Profesa Hozen Mayaya amesema  Rais ametekeleza kwa ufanisi miradi ya kimkakati na kutoleta mfano ushiliki wa filamu ya Royal tour ambao umeongeza idadi ya watalii wanaokuja kutembelea nchini na kazi kubwa ya wananchi ni kuendelea kumuombea.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Umoja wa Vyuo vya Mashariki na Kusini mwa Afrikia ( ESAURP) Ruta Mutakyawa alitumia nafasi hiyo kusema  kuwa walisimamia uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho ambapo kitabu kina kurasa 624 ,sura 29.

Mbali na hayo ameeleza  kuwa kitabu hicho  kimewashirikisha wadau 45 waliotoka vyuo vya elimu ya juu, mashirika ya umma na asasi za kiraia.

Katika uzinduzi huo Waziri wa Elimu Profesa Aldof Mkenda ameipongeza ESAURP ambao ndio wamechapisha kitabu hicho kwa uandishi na uchapishaji wa vitabu vingi ambavyo vimekuwa vikifundisha na kuelimisha jamii.

Amesema,Serikali kupitia wizara hiyo ipo mbioni kuanzisha mfuko rasmi wa kuwasaidia waandishi mahiri wa vitabu huku akiwataka  waandishi wote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa ili kutoanmaaandiko makini yatakayoleta tija kwennye jamii.

Waziri Mkenda amesema katika uongozi wa Rais Samia  umuhimu wa uandishi umeonekana na Serikali kuona haja ya kufanya kwa vitendo kwa kuanzisha tuzo ya Mwalimu Nyerere  ili waandishi nguli na mahili kuweza kushiriki na kujipatia tuzo hizo

" Katika kitabu hiki nimeona kimeandikwa na waandishi wengi na ndani yake kinavitu vingi niitake jamii ya watanzania kukisoma na kujua mambo mengi yanayohusu utendaji wa Rais Samia,"amesema.

Kutokana na hayo mmoja wa Mwandishi wa kitabu hicho Profesa Ted Maliyamkono alisema kulikuwa na kila sababu ya kuandika kitabu hicho kwa kushirikisha watu mbalimbali ili kuwaeleza watanzania na dunia kwa ujumla mambo mengi na mazuri yanayofanywa na Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika kitabu hicho walizingatia mambo muhimu ya Kisera na sio kufanya tathmini ya utawala wake na kuwataka wananchi wasione udhaifu  wa kitabu.

Vilevile alitaja  lengo kuu la chapisho hilo kuwa ni kuchangia uboreshaji wa Sera serikaini.

" Ndani ya kitabu hiki kinaonyesha Rais Samia amekuwa wa kwanza kutembelea nchi nyingi tofauti na wengine  ili kufunga njia zilizofungwa na milango ya biashara,pia amekuwa Rais wa kwanza kufanya Royal tour na amekuwa Mtendaji wa vitendo na sio wa maneno," amesema Mwandishi huyo .

Amefafanua kuwa katika utawala wa Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza kuteua mawaziri wawili Wanawake katika Wizara mbili ambazo hazikuwahi kuongozwa na wanamke enzi na enzi ambazo ni Wizara ya Ulinzi na Wizara  ya Mambo ya Nje.

"Rais Samia pia ameendeleza kazi yote iliyoachwa na Rais wa awamu ya tano hayati John Magufuli na kuhakiki Katiba mpya na kuona atashughulikia kwa namna gani na kwa wakati ulio sahihi,"amesema


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments