MWENZETU AGOMEA MATOKEO YA UCHAGUZI TENA SHINYANGA NGELELA AKIENDELEA KUTINGISHA


Edward Ngelela (kushoto) akiwa katika uchaguzi wa awali akitetea kiti chake cha Uenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini, (wa pili kutoka kulia) ni Mwenzetu Mgeja naye akiwania nafasi hiyo, ambapo katika uchaguzi wa marudio ameshindwa tena na kugoma kusaini matokeo.

Wajumbe wakipiga kura.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela, ambaye ametetea kiti chake kwa kupata ushindi wa kishindo.

Na Halma Khoya ,SHINYANGA

CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kimefanya uchaguzi wa marudio kwa nafasi ya Mwenyekiti, pamoja Katibu wa Itikadi na Uenezi, mara baada ya uchaguzi wa awali kuingiwa na dosari.

Uchaguzi huo umefanyika Jana katika Uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga, ambapo uchaguzi wa awali ulifanyika Oktoba Mosi mwaka huu, na Edward Ngelela alitangazwa kushinda nafasi ya Uenyekiti, pamoja na Emmanuel Lukanda kushinda nafasi ya Uenezi.

Katika uchaguzi huo wa marudio, Edward Ngelela ametangazwa kushinda tena nafasi ya Uenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini kwa kupata kura 741, akifuatiwa na Mwenzetu Mgeja kura 157, Peter Kawiza kura 48, na Anna Ng’wagi kura 11.

Aidha, kwa upande wanafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Emmanuel Lukanda, ameshinda tena nafasi hiyo kwa mara ya pili kwa kupata kura 120, akifuatiwa na Mohamed Hussein kura 10 na Rojas Samsoni kura Tatu.

Hata hivyo katika uchaguzi huo wa marudio Mmoja wa Wagombea wa nafasi ya Uenyekiti Mwezetu Mgeja, aligoma kusaini matokeo hayo kwa madai kuwa uchaguzi huo umegubikwa na figisu figisu.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmad Salum, amesema uchaguzi huo umekuwa wa demokrasia na haki, na amewaomba viongozi wawe na ushirikiano ili kuleta maendeleo ya ndani na nje ya chama.

"Uchaguzi umekuwa wa haki kwa kila mtu na hakuna ubishi wowote uliotokea na washindi wamepatikana, kinachofuata sasa ni kuchapa kazi kwa ushirikiano,”amesema Salum.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments