RAIS AZUA TAHARUKI KUMTEUA MAREHEMU KUWA KAMANDA WA POLISI


Jenerali Floribert Kisembo Bahemuka alifariki mnamo Mwaka 2011 kwa kupigwa Risasi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Félix Tshisekedi

HALI ya sintofahamu imejitokeza Katika Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) baada ya Rais Félix Tshisekedi kumteua Jenerali Floribert Kisembo Bahemuka aliyefariki mnamo Mwaka 2011 kwa kupigwa Risasi kwa kudaiwa kuunda kikundi cha Uasi dhidi ya Serikali, kuwa mmoja wa Makamanda wa Jeshi.


Mwendazake Jenerali Floribert Kisembo Bahemuka alikuwa kamanda wa Kikosi cha FARDC huko e in Lubutu, Maniema na alipigwa risasi na kufariki dunia Aprili 30, 2011 na kikosi cha Serikali huko Lonyo village, Djugu.


Genera Floribert Kisembo alikuwa pia kamanda mwandamizi wa kikosi cha UPC chini ya Thomas Lubanga.

Rais Tshisekedi ambaye alifanya uteuzi huo juzi Jumatatu, Oktoba 17, 2022, pia alimtaja Jenerali aliyetoroka Jeshini, Jenerali John Tshibangu kama Kamanda wa eneo la 21 la Kijeshi katika uteuzi huo mpya.

Jenerali Tshibangu Mwaka 2011 aliondoka Jeshini na kuongoza Uasi dhidi ya utawala wa Rais Joseph Kabila baada ya madai ya wizi wa kura kutoka eneo la Kasai Mashariki.



Tshibangu alikuwa miongoni mwa makamanda waliokuwa wakimuunga mkono kiongozi wa upinzani wakati ule, marehemu Étienne Tshisekedi ambaye ni baba mzazi wa Rais wa sasa wa Congo, Felix Tshisekedi.


Baadaye alikimbilia Tanzania kama mkimbizi wa kivita kabla ya kurejeshwa Kinshasa kukabiliana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili kuhusu uasi dhidi ya Serikali ya Kabil.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments