JESHI LA POLISI LAWATAKA WAZAZI KUONGEA NA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI TARIME



Sp Fatma Mbwana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mangucha katika ufunguzi wa mashindano hayo
Sp Fatma Mbwana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mangucha katika ufunguzi wa mashindano hayo
Valerian Mgani meneja miradi ATFGM Masanga akiongea na wananchi wa kijiji cha Mangucha katika ufunguzi wa mashindano hayo.
Valerian Mgani meneja miradi ATFGM Masanga akiongea na wananchi wa kijiji cha Mangucha katika ufunguzi wa mashindano hayo.
Valerian Mgani meneja miradi ATFGM Masanga akiongea na wananchi wa kijiji cha Mangucha katika ufunguzi wa mashindano hayo.

**


Na Frankius Cleophace -Tarime Mara

Jeshi la Polisi wilaya ya Polisi Nyamwaga limewasihi wazazi na walezi kujenga mazoea ya kuongea na watoto wao ili kuweza kubaini vitendo vya ukatili ikiwemo ulawiti.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu kituo cha polisi wilaya ya Kipolisi Nyamwaha SP Fatma Mbwana katika uzinduzi wa tamasha la michezo lilolenga kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili.

Fatma alisema kuwa wazazi wawe na mazoea ya kuongea na watoto wao wadogo hususani kuanzia miaka 0-8 kwa lengo la kutambua hali zao kwani vitendo vya ukatili vinazidi kuongezejka hapa Nchini.

“Wazazi kazi yetu nikuamka na mabeseni ya ndizi kwa ajili ya kufanya biashara baba yuko ‘busy’ sana muda wa kukaa na watoto hatuna baadhi ya wachungaji sasa nao wameanza matukio mabaya sasa tunapaswa kulinda watoto wetu”, alisema Fatma.

Pia Fatma aliwasihi walezi kulea watoto wao katika malezi bora ili kuwa na kizazi chenye kujitambua.

Valerian Mgani ambaye ni meneja miradi kutoka asasi ya ATFG Masanga ambao wameandaa tamasha la michezo kwa lengo la kutoa elimu alisema kuwa tamasha hilo limelenga kufikisha elimu ya kupinga ukatili wa aina yeyote katika jamii.

“Timu Nane kutoka kata nane zote zinashiriki mashindano hayo kabla ya michuano viongozi wa serikali wakiwemo jeshi la polis lazima watoe elimu ili kupinga ukatili wa kijinsia ukiwemo Ubakaji, Ulawiti kwa watoto, vipigo kuchomwa moto na suala la ukeketaji”, alisema Valerian.


Emanuel Samsoni Mkazi wa kijiji Mangucha Tarime alisema kuwa serikai ionea haja kubwa ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya matukio ya ulawiti kwa watoto kwani jamii haina elimu juu ya ukatili huo.

Petro Mseth ambaye ni Afisa Mtendaji Kijiji Mangucha alisema kuwa katika kipindi cha mwaka huu hajapokea taarifa zozote zinazohusu masuala ya ulawiti kwa watoto nakuomba jamii kuendelea kutoa taarifa juu ya matukio ya ukatili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments