HUDUMA ZA AFYA ZAANZA KUTOLEWA HOSPITALI MPYA YA RUFAA MKOA WA SHINYANGA ILIYOPO MWAWAZA

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKOA wa Shinyanga umeelezea mafaniko makubwa katika sekta ya afya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha huduma za afya mkoani humo hadi kufikia hatua ya kuhamia rasmi katika Hospitali mpya ya Rufaa iliyopo Mwawaza Manispaa ya Shinyanga.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu ameelezea mafanikio hayo leo Septemba 8, 2022 wakati akizungumza na vyombo vya habari.

Amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia, imefanya mambo makubwa katika Sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu, ikiwamo na ujenzi wa Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

“Tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za Afya hapa nchini ukiwamo na Mkoa wa Shinyanga, ambapo tumepata fedha nyingi na tumejenga majengo mengi yakiwamo ya huduma ya dharura, mlipuko wa Magonjwa, Wagonjwa Mahututi, pamoja na jengo la kuzalisha hewa ya Oksijeni,”amesema Mulyutu.

Aidha, amesema pia katika kuboresha huduma hizo za afya mkoa wa Shinyanga umefikia hatua ya kuanza kuhamia rasmi kwenye Hospitali yake mpya ya Rufaa mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga na huduma zimeanza kutolewa, na kumpongeza Rais Samia kwa kuijali Sekta ya Afya na kuimarisha Afya za wananchi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu akizungumza na waandishi wa habari na kuelezea mafanikio ya Sekta ya Afya awamu ya Sita. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments