PANYA ROAD WAUA NA KUJERUHI DAR


Maria Baso, aliyeuawa na panya road

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Maria Baso mwenye umri wa miaka 20, anadaiwa kuuawa katika tukio la uvamizi lililofanywa na vijana zaidi ya 30 wanaodhaniwa kuwa ni panya road huku wengine wawili wakijeruhiwa.


Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia Septemba 14, 2022, eneo la Kawe Mzimuni jijini Dar es Salaam, ambapo vijana hao pia wamepora vitu mbalimbali ikiwemo simu na fedha.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wameeleza namna tukio hilo lilivyotokea huku mama mzazi wa Maria anayedaiwa ameeleza kusikitishwa kwake kwa vijana hao kutochukuliwa hatua na kukamatwa kwa kuwa wameendelea kuleta taharuki kwa wananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments