TANZANIA YAZUNGUMZIA MADAI YA EU MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU…."TUMEFUATA TARATIBU ZOTE"


Muonekano wa moja ya nyumba za mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, Mzee Kazimila Patrick Mshandete mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora aliyejengewa nyumba za kisasa baada ya kukubali kupisha eneo lake kwa ajili ya mradi huo wa mafuta. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Muonekano wa moja ya nyumba za mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, Mzee Kazimila Patrick Mshandete mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora aliyejengewa nyumba za kisasa baada ya kukubali kupisha eneo lake kwa ajili ya mradi huo wa mafuta.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio ( wa pili kushoto) akizungumza na Mzee Kazimila Patrick Mshandete (kulia) mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora ambaye ni mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga. Mwananchi huyo alikubali kutoa eneo lake la hekari 6 kwa ajili ya kupisha mradi huo ambapo Serikali imemlipa fidia na kumjengea nyumba za kisasa na kuendelea kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kila mwezi.
Mzee Kazimila Patrick Mshandete (kulia) mkazi wa kijiji cha Sojo kata ya Igusule wilaya ya Nzega mkoa wa Tabora ambaye ni mnufaika wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga akiishukuru serikali kumjengea nyumba za kisasa na kupongeza jinsi mradi huo unavyotekelezwa kwa uwazi na kuzingatia haki za binadamu.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi (katikati) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) kuhusu ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) akizungumza wakati akikagua ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Kaimu Meneja wa Kiwanda cha Kufunika mabomba katika kijiji cha Sojo, William Kajagi (katikati) akimwelezea Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kushoto) kuhusu ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga.
Muonekano maendeleo ya ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Muonekano maendeleo ya ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio (kulia) akizungumza wakati akikagua ujenzi wa msingi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.
***

Kadama Malunde & Mitandao

Serikali ya Tanzania imesema ya kwamba miradi yote mikubwa inayotekelezwa nchini humo inafuata sheria na kanuni za kimataifa ikiwemo za utunzaji wa mazingira na kuheshimu haki za binadamu huku ikifanya miradi yake kwa manufaa ya wananchi wake.


Waziri wa Nishati, Januari Makamba ametoa kauli hiyo Ijumaa Septemba 16, 2022 ikiwa ni sehemu ya ufafanuzi ya maazimio yaliyotolewa siku tatu na Bunge la Ulaya (EU) kuhusu utekelezaji wa mradi huo.


Waziri wa Nishati nchini Tanzania, Januari Makamba amesema hakutakuwa na athari zozote za kimazingira wakati wa utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha Mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga kwani tahadhari zote zilizingatiwa kitalaamu.


Makamba amesema Tanzania inazingatia vigezo vya kimataifa katika miradi yake ikiwemo ule wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Tanga nchini Tanza na kwamba hakuna kinachokiukwa kama azimio la bunge hilo linavyoeleza.


Makamba amesema, “Nimefuatilia mapendekezo na Azimio la Bunge la Umoja wa Ulaya kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu na uharibifu wa mazingira, Nimeona wameshauri juu ya mradi na athari zake. Serikali ya Tanzania imefuata taratibu zote za kuhakikisha haki za watu na mazingira zinalindwa lakini hakuna kilichokiukwa...


"Tumelipa fidia wananchi wote ambao maeneo yao yapo kwenye eneo la mradi, hakuna yoyote aliyelazimishwa au kukamatwa kwa nguvu. Lakini pia tumefuata kanuni zote zinazohusu mazingira ili mradi huu usidhuru mazingira.


"Kilichopo ni kuwa Tanzania ina kila haki ya kuhakikisha wananchi wake wananufaika na rasilimali zilizopo kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea ambazo wananchi wake wananufaika na miradi hiyo", amesema Waziri Makamba.



Wakati huo huo, Bunge la Uganda limelaani azimio la bunge la Umoja wa Ulaya linalozitaka Uganda na Tanzania kusitisha maendeleo ya miradi yao ya mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika kikao cha Alhamisi, Naibu Spika wa Uganda Thomas Tayebwa alisema azimio hilo linatokana na taarifa potofu na upotoshaji wa makusudi wa mambo muhimu kuhusu mazingira na ulinzi wa haki za binadamu.

Alisema inawakilisha kiwango cha juu kabisa cha ukoloni mamboleo na ubeberu dhidi ya Uganda na mamlaka ya Tanzania.

Septemba 16,2022, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga na kujionea shughuli mbalimbali za ujenzi wa Kiwanda cha kufunika Mabomba (Themo Isolation) katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilaya ya Nzega mkoani Tabora.


Dk. Mataragio amefanya ziara hiyo katika kambi ya kijiji cha Sojo kata ya Igusule pamoja na kumtembelea mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Kazimila Patrick Mshandete ambaye alikubali kutoa eneo lake kwa ajili ya kupisha mradi huo ambapo Serikali imemlipa fidia na kumjengea nyumba za kisasa na kuendelea kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kila mwezi.


Akizungumza katika Kambi hiyo ya Sojo, Dk. Mataragio alisema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Mradi huo ambapo kazi za awali za ujenzi wa Kiwanda cha Kufunika Mabomba zimefikia 60% huku akieleza kufurahishwa zaidi kuona fursa mbalimbali za ajira zikitolewa kwa wananchi wazawa wanaozunguka mradi huo.


Akiwa katika makazi mapya ya mnufaika wa mradi huo, Kazimila Patrick Mshandete mkazi wa kijiji cha Sojo ambaye ni miongoni mwa wakazi zaidi 300 waliopisha maeneo yao kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, Dk. Mataragio amesema imelipa fidia kwa wananchi na wengine kuwajengea nyumba za kisasa huku akibainisha kuwa taratibu zote zikiwemo za kimataifa zimezingatiwa.


“Tumefuata taratibu zote, tumewalipa fidia na kuwajengea nyumba za kisasa hivyo hakuna ukiukwaji wowote wa haki za binadamu. Tunatekeleza Mradi huu kwa uwazi mkubwa na tunazingatia haki za binadamu, hakuna haki inayokiukwa”,alieleza Dk. Mataragio.


Mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Kazimila Patrick Mshandete alisema tangu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta uanze kumekuwa na ushirikishwaji wa wanakijiji hatua kwa hatua na kwa uwazi na wananchi wameshalipwa fidia na wale waliotaka kujengewa makazi wameshajengewa nyumba za kisasa na wanapatiwa huduma mbalimbali ikiwemo chakula kila mwezi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments