TBS YATOA MAFUNZO YA UDHIBITI SUMUKUVU KWENYE MAZAO JIJINI TANGA

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Hashim Mgandilwa akifungua mafunzo kuhusu udhibiti wa Sumukuvu kwa mazao ya mahindi, karanga, Viungo vya chakula pamoja na bidhaa zake kwa wajasiriamali kutoka katika Jiji la Tanga. Meneja wa Mafunzo na Utafiti TBS, Mwl.Hamisi Mwanasala akizungumza kwenye Ufunguzi wa mafunzo kuhusu udhibiti wa Sumukuvu kwa mazao ya mahindi, karanga, Viungo vya chakula pamoja na bidhaa zake kwa wajasiriamali kutoka katika Jiji la Tanga. Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Bi.Sipora Jonathan akizungumza katika Ufunguzi wa mafunzo kuhusu udhibiti wa Sumukuvu kwa mazao ya mahindi, karanga, Viungo vya chakula pamoja na bidhaa zake kwa wajasiriamali kutoka katika Jiji la Tanga. Naibu Meya wa Jiji la Tanga Bw.Joseph Colvas akizungumza katika Ufunguzi wa mafunzo kuhusu udhibiti wa Sumukuvu kwa mazao ya mahindi, karanga, Viungo vya chakula pamoja na bidhaa zake kwa wajasiriamali kutoka katika Jiji la Tanga. Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Hashim Mgandilwa akipata picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa viwango katika Ufunguzi wa mafunzo kuhusu udhibiti wa Sumukuvu kwa mazao ya mahindi, karanga, Viungo vya chakula pamoja na bidhaa zake kwa wajasiriamali kutoka katika Jiji la Tanga.

****************

NA MWANDISHI WETU

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe.Hashim Mgandilwa amelipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa jitihada inazozifanya za kuendesha mafunzo kwa lengo la kuelimisha wajasiriamali na umma kwa ujumla juu viwango na ubora wa bidhaa hususani bidhaa za chakula.

Ametoa pongezi hizo leo tarehe 29/03/2022 wakati akifungua mafunzo kuhusu udhibiti wa Sumukuvu kwa mazao ya mahindi, karanga, Viungo vya chakula pamoja na bidhaa zake kwa wajasiriamali kutoka katika Jiji la Tanga.

Amesema Umuhimu wa chakula unasababisha suala la usalama kupewa kipaumbele katika kulinda afya ya jamii na uchumi wa nchi na kuwa kigezo muhimu katika biashara ya kitaifa na kimataifa.

"Chakula kisicho salama husababisha madhara ya kiafya na hata vifo kwa walaji pamoja na kusababisha athari za kiuchumi. Hata hivyo, usalama wa chakula unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa sumukuvu ambayo husababisha madhara ya kiafya na hata kiuchumi". Amesema

Aidha amewasihi wasindikaji na wazalishaji wa mazao kuzingatia mikakati ya kukabiliana na changamoto ya sumukuvu ili vyakula vyetu viendelee kuwa salama kwa muda wote.

Kwa upande wake Meneja wa Mafunzo na Utafiti Mwl.Hamisi Mwanasala amesema mafunzo hayo ni mojawapo ya fursa muhimu ya kuelimisha jamii juu ya kukabiliana na sumukuvu ili kulinda afya za wananchi na kuwezesha biashara ya chakula.

"Ili kuimarisha usalama wa chakula dhidi ya sumukuvu, TBS inatekeleza mikakati mbalimbali, ikiwemo udhibiti wa sumukuvu kwenye chakula hususani mazao ya mahindi, karanga na viungo vya chakula ambayo ndiyo yenye uwezekano mkubwa wa kuchafuliwa na sumukuvu". Amesema Mwl.Mwanasala.

Amesema TBS inatoa elimu kwa wadau katika mnyororo wa thamani wa mazao ya chakula kwani jamii ikielimika itatoa mchango zaidi katika kukabiliana na sumukuvu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments