WAZIRI SIMBACHAWENE ATANGAZA MSAMAHA KWA WAMILIKI WA SILAHA KINYUME CHA SHERIA KAMA WATAJISALIMISHA


WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene

Na Dotto  Kwilasa, Dodoma

WAZIRI wa Mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene ametangaza msamaha wa kutoshitakiwa wale wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria iwapo watasalimisha silaha hizo haramu kwa hiari na kwa muda uliopangwa.

Simbachawene amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu tangazo la msamaha na usalimishaji wa silaha kwa wanaomiliki kinyume na sheria huku akisisitiza kuwa hali hiyo itasaidia udhibidi na uzagaaji wa silaha hizo mitaani.

Waziri huyo amesema,hatua hiyo ni moja ya makubaliano ya Umoja wa mataifa yaliyofanyika mwezi Julai 2018 kuhusu udhibiti wa uzagaaji wa silaha haramu duniani na kusababisha uvunjifu wa amani,ukosefu wa usalama,hofu Kwa watu,vifo na majeruhi.

"Kwa kuzingatia misingi ya maadhimio ya Umoja wa mataifa,Umoja wa Afrika na sheria za usimamizi na udhibiti silaha na risasi ya mwaka 2015,sura ya 223 na kanuni zake za mwaka 2016 na kwa mamlaka niliyopewa nawasihi wamiliki wote wa silaha kichume na sheria kuhakikisha wanatekeleza zoezi hili ipasavyo,"amesema.

Kwa mujibu wa Waziri huyo mwenye dhamana ya Mambo ya ndani ya nchi,zoezi hilo la usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari litafanyika kuanzia tarehe 2/11/2021 hadi 30/11/2021 kwa nchi nzima na kwamba silaha hizo zisalimishwe kwenye vituo vyote vya Jeshi la polisi na Ofisi za Serikali za mitaa kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.

"Nasisitiza kwamba baada ya muda uliowekwa kupitia,msako mkali utafanyika Kwa Nchi nzima kiwabaini na kiwakamata wote wanaokaidi nafasi hii ya msamaha ,nawakumbusha kuwa zaoezi hili ni la mwezi Novemba tu hivyo wakaidi wote tutawachukulia Kama watuhumiwa ,"amesema Simbachawene.

Licha ya hayo amewataka wananchi wote ambao ndugu zao walikuwa wanamiliki silaha kihalali na sasa wamefariki,kuhakikisha wanasalimisha silaha hizo huku akiwataka wamiliki wote wa silaha nchini kuendelea kuchukua tahadhali dhidi ya matumizi mabaya .

Kutokana na hayo amelitaka Jeshi la polisi nchini kuandaa mpango kazi wa kila siku wa kukusanya silaha zitakazosalimishwa katika Serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya jumla mara zoezi hilo litakapokamilika.

"Niwaombe pia Viongozi wa mitaa na watendaji wa kata kutengeneza mazingira ya kiwapokea wananchi wote watakaokubali kwa hiari kuja kusalimisha silaha zao,katika hili tekelezeni sheria vizuri,"amesisitiza

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments