NATO KUKUTANA KWA DHARURA LEO BAADA YA WANAJESHI 33 WA UTURUKI KUUAWA SYRIA


Baraza la kiutawala la Jumuia ya Kujihami ya NATO linakutana leo katika kikao cha dharura kuhusu mzozo wa Syria, baada ya wanajeshi wapatao 33 wa Uturuki kuuawa katika shambulizi la anga huku wengine wengi wakijeruhiwa vibaya.


Baraza hilo ambalo linawajumuisha mabalozi wa nchi zote 29 za NATO wanakutana baada ya Uturuki kuomba mazungumzo yafanyike chini ya kifungu cha 4 cha Mkataba wa NATO, kuhusu hali ya Syria. 

Kulingana na kifungu hicho, mwanachama yeyote wa NATO anaweza kuomba mazungumzo yafanyike iwapo ataamini kuwa kuna kitisho katika uhuru wake wa kisiasa au usalama. 

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg ametoa wito wa mapigano kusitishwa na amelaani mashambulizi ya anga katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527