KUTANA NA MWANAMME HUYU WA AJABU,TANGU AZALIWE HAJAWAHI KUONANA NA MWANAMKE,HATA KUSHIKANA TU MIKONO

SUTI 2 

Tokyo ni moja kati ya miji maarufu inayofahamika kwa kuwa na huduma ya karibia kila hitaji la mwanadamu duniani, unaweza usiamini ila Tokyo iliyopo ndani Japan ni nchi inayoongoza kwa kuwa na kila huduma inayokidhi mahitaji ya kimapenzi duniani kitu ambacho kinaweza kukufanya uione Japan kama ni walevi wa mapenzi. 

Lakini fikra hizi zinaweza zikabadilisha mtazamo wako kuhusu nchi hii pale utakapokutana na Takashai Sakai mwanaume mwenye miaka 41 ambaye hajawahi kukutana na mwanamke toka azaliwe.

Akiwa katika miaka ya 40 na zaidi mwanaume huyu hajawahi kabisa kukutana na mwanamke, kushikana mikono wala kumkumbatia mwanamke yoyote.
 
 Lakini Takashai hayuko peke yake nchini Japan, kwani utafiti unaonyesha kwamba moja kati ya wanaume wanne wakijapan kwenye rika la miaka 30 hadi 40 hawajawahi katika maisha yao kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi, kushiriki tendo la ndoa wala kuoa!
 
 baadhi wakiwa wameanua kuishi maisha ya namna hiyo ila kwa wengi waliopo hali hii haikuwa chaguo lao bali walijikuta tuu hawawezi, na wangependa hali hii ibadilike kwani wanatamani kuonja ulimwengu huo sasa.
 TOOKYO 2
Lakini kwa asilimia kubwa ya wanaume wenye hali hii Japan darasa la uchoraji wa watu wakiwa hawajavaa nguo ambalo linaitwa “Nude Art Class” .. hili ni suluhisho dogo kwa uhalisia walio nao na kwa upande wa pili ni fursa pekee walionayo kumuona mwanamke akiwa mtupu!! Mmoja ya walimu wa vipindi hivyo alisikika kwenye interview fupi akisema;
 
>>> “madarasa kama haya hujaribu kuwasaidia watu kama hawa kuenjoy uumbaji wa jinsia ya kike kupitia uchoraji, tunafanya hivi kuijenga saikolojia ya wanaume hawa kuwaona wanawake sio watu wa kuwaogopa na hatimaye kuvunja uwoga wao wa kufanya mapenzi, hii ndio dhamira yetu”.
 
Watafiti wamesema ongezeko la wanaume wenye shida hii imekua ikionekana kama kikwazo kwa ukuwaji wa nchi kwasabau idadi ya wanaume hawa inavyo ongezeka, idadi ya uzaaji unapungua na hatimae kupunguza idadi ya watu nchini. Hili linaoneka kua kama janga kwa moja ya nchi yenye uchumi mkubwa duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم