WATU SABA WAFARIKI BAADA YA KUNYWA POMBE YA KIENYEJI...WALIANZA KWA KUUMWA VICHWAHii sio mara ya kwanza kupata stori kutoka Kenya kuhusu pombe ya kienyeji kuua watu, imeingia kwenye headlines tena leo June 24 2015 ambapo watu saba wamefariki na wengine wamelazwa Hospitali baada ya kunywa na pombe ya kienyeji.

Baada ya kunywa pombe hiyo walianza kutetemeka na wengine wakashindwa kutembea, hii ikafanya watu wa Usalama kuingia mtaa mmoja baada ya mwingine katika Kaunti ya Kiambu, Kenya.

“Macho yalianza kuuma, nikaanza kuumwa na tumbo” >>> aliongea mmoja watu waliokunywa Pombe hiyo na kuzidiwa.

Mtu mwingine nae anasimulia; “Nilivyokunywa nilijisikia tu ulevi wa kawaida, baadae usiku nikajisikia kutetemeka”

Watu hao walikutwa wakiwa na hali mbaya pembeni ya barabara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم