KUTANA NA KONDOMU HIZI ZENYE UWEZO WA KUTAMBUA MAGONJWA YA ZINAA MNAPOFANYA MAPENZI

mipiraa

Wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Uingereza wamezindua mipira ya kiume ‘kondomu’ yenye uwezo wa kugundua maradhi ya zinaa wakati watumiaji wanapokutana kimwili.
Kondomu hiyo inayojulikana kama S.T.EYE inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
mipira
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria waliopo kwa muhusika.
Kutukana na kuvumbua mipira hiyo wanafunzi hao tayari wametunukiwa tuzo ya ubunifu na kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia ya ‘the TeenTech’ pamoja na pauni 1,000.
Wanafunzi hao wamesema wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kusaidia vizazi vijavyo ili kuepukana na maradhi yanayoweza kuzuilika kitaalam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527