TAZAMA PICHA- HATIMAYE LUNDO LA KINYESI NA MATAPISHI YA MWALIMU WA DAR ALIYOHIFADHI CHUMBANI MIAKA 2 YATEKETEZWA


Manispaa ya Temeke jana imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.


Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani.


“Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo tulichukua jukumu la kwenda kumhoji Mkuu wa wa shule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza kuwa alikuwa na akili timamu,”alisema Tembo. 

Alisema pamoja na kuuteketeza mlundikano huo wa kinyesi pamoja mikojo na matapishi bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.

“Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine ingawa hatuwezi kuamini mambo ya ushirikina lakini haiwezekani mwalimu kama yule ajisaidie na kuhifadhi uchafu kama ule ndani,”alisema.


Aidha, alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uaangalizi wa polisi.

Tembo, alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Haspitali ya Taifa muhimbili kwa ajili ya kupimwa afya baada ya kupata mshituko ambao umesababishwa na taarifa hizo.

Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira, Jumamne Muhogo, alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mikojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika.

Pia alisema kipo kifungu cha sheria, walifika pale maofisa kutoka idara mbalimbali kupima uzito wa tukio, ambapo kama wangemkuta wangemkamata kwa hatua za kumfikisha mahakamani.

 
Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza mahakamani.

“Tukio hili kwa manispa ya Temeke ni la kwanza kutokea yaani inaekekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili za kawaida asingeweza kufanya namna hii,”alisema.


Umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo walikusanyika kwa wingi tangu saa tatu asubuhi wakisubiri kazi hiyo hadi ilipofanyika saa tisa alasiri na wataalamu wa manispaa hiyo.

Wataalamu hao walimwagia dawa uchafu huo kisha kuanza kubeba na kutumbukiza chooni kwa uangalifu mkubwa.

 
Walipomaliza walvisafisha vyombo hivyo kwa kutumia dawa ambazo zimeweza kusaidia kuondoa harufu mbaya iliyokuwa imezagaa hewani.

Awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi  Ramadhan Kagolo, alisema aliwajibika kusimamia kuvunjiwa kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii.

Tukio hilo ambalo limekuwa likifuatiliwa na majirani hususan jana wakati wa uteketezaji lilitokea Februari 22 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527