TAZAMA PICHA- HII NDIYO SEHEMU AMBAYO MAREHEMU RACHEL HAULE WA BONGO MOVIE NA MWANAYE WATAPUMZIKA DAIMA MILELE

RECHO: Hapa ndipo atakapo anza siku yake ya kwanza leo kwenye makazi yake mapya mbinguni. Shimo dogo ni kaburi la mtoto wake aliyefariki muda mfupi baada ya kumzaa katika hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam!


RECHO: KUZALIWA 1988  KUFARIKI: 2014. UMRI:miaka 26
Mwili wa marehemu Recho aliyekuwa msanii wa bongo muvi na mwili wa mtoto wake kwa sasa unatolewa katika hospitali ya taifa muhimbili na kupelekwa nyumbani kwao Sinza, na baadaye viwanja vya leaders club kwa ajili ya kuagwa.

Kwa mujibu wa mwanahabari Zamaradi Mketema ni kuwa miili hiyo ya marehemu (Recho na mwanaye itaagwa na ndugu wa karibu kwa dakika chache nyumbani kwao Sinza na kwenda viwanja vya leaders.


Tukio hilo limeleta simanzi kwa ndugu jamaa na marafiki na vilio ndiyo vimetawala kwa wasanii wa bongo muvi waliofika hospitali ya  Muhimbili na kuchukua marehemu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527