Mauaji ya Kutisha!! MWENDESHA BODABODA ACHINJWA KAMA KUKU NA MAJAMBAZI,PICHA ZA MAJAMBAZI ZIKO HAPA TAZAMA 
 

Pichani ni mmoja kati ya watu 3 wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo,picha za wengine ziko hapo chini tazama.

Jeshi la Polisi Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kumuuwa dereva Bodaboda mmoja aitwaye Frenk Joseph (25)mkazi wa mtaa wa Nsemlwa Wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi kwa kumchinja shigo na kisha kumpora pikipiki yake aina ya SANLG yenye namba za usajiri T 704 CDQ.

Kamanda wa jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Charles Kidaha(29),Madia Mtema (40) na Buyenza Jendesha (40) wote wakazi waTarafa ya Mwese Wilayani Mpanda. 

(Picha zote 3 ni za wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم