WIVU WA MAPENZI WAUA HUKO MBEYA,MUME AUA MKE

Mwanamke mmoja  aliyetambuliwa kwa jina la Christina Hayola(35), mkazi wa Kijiji cha Lwalanje wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, amekutwa amekufa na mwili wake kubainika kuwa ulikuwa na majeraha ya kukatwa katwa Kifuani, kichwani na mguu wake wa kulia.
 
Unyama huo unadaiwa kufanywa na mumewe, Mussa Nsagaje, maarufu kwa jina la Mwaulambo.

Sababu za mauaji hayo zinatokana na kile kinachodaiwa kuwa  ni ugomvi wa masuala ya wivu wa kimahusiano(Ngono) ulioanzia eneo la kilabu cha pombe.
 
Mwili wa marehemu ulikutwa katika Kijiji cha Magamba, kata ya Isansa, tarafa ya Igamba, wilayani Mbozi, mkoani Mbeya na mtuhumiwa alitoroka baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم