MGEJA AKUSANYA MAMILIONI YA PESA KATIKA HARAMBEE YA UJENZI WA KITUO CHA POLISI- DIDIA WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI

Muda mchache tu baada ya kuwasili katika eneo kunakojengwa kituo cha polisi katika kijiji cha Didia kata ya Didia wilaya ya Shinyanga vijijini,katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja akiingia ndani ya jengo linaloendelea kujengwa

Ndani ya jengo la kituo cha polisi Didia kinachoendelea kujengwa kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama wa raia na mali zao kutokana na wafanyabiashara kuanza kuvamiwa kwa nguvu kila mara tangu mwaka 2008,wakioprwa na kuuawa kinyama

Kulia ni D/SGT Joseph Mandahu,mwakilishi wa mkuu wa kituo cha polisi cha Tinde akitoa maelezo kuhusu ujenzi huo unaondelea ambapo wafanyabiashara wa Didia wamejitolea kuchangia ujenzi wa kituo hicho ili kuisaidia serikali kufikia malengo haraka

Ndiyo hali halisi ya ujenzi ulipofikia katika kijiji cha Didia ambacho kinakaliwa na wafanyabiashara wengi

Aliyesimama ni katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini ndugu Mahamud Suleiman akimkaribisha mheshimiwa Hamis Mgeja katika kikao cha harambee ya ujenzi wa kituo cha polisi cha Didia ambapo zinahitajika shilingi 11,910,000/= hadi kukamilika ujenzi huo.Pembeni ni mh Mgeja,wa kwanza kushoto ni mwenyekiti wa CCM kata ya Didia Peter Sheliya Kashinje akifuatiwa na mwenyekiti wa kijiji cha Didia bi Siyumba Idd.

Kikao kinaendelea kushoto ni mwenyekiti wa chama cha wakulima wa pamba Tanzania Elias Mayiku Zizi,kulia ni katibu wa Chama hicho bwana George Mpanduji wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Ndugu Msanii  Richard Masele ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Shinyanga vijijini akiwasalimu wakazi wa Didia ndani ya kikao hicho ambapo alisema uwepo wa kituo cha polisi mahali hapo kutapunguza uhalifu ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara eneo hilo

Katibu wa kamati ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi bwana Kagera Chacha akisoma risala juu ya ujenzi huo katika kijiji cha Didia chenye kaya 1008 na jumla ya wakazi 4788,wanaumme 2297 na wanawake 2491 wengi wao wakiwa ni wakulima hasa zao la mpunga na wafanyabiashara ndogo ndogo

Awali Diwani kwa kata ya Didia ndugu Luhende Paul  Masele akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ujenzi huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM na kwamba kituo hicho cha polisi kitachangia kuwepo kwa amani katika eneo hilo kwani wafanyabiashara wamekuwa wakivamiwa na kuuawa na hivi karibuni kuna mfanyabiashara aliuawa kwa kupigwa risasi

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Mahamud Suleiman akionesha ilani ya ccm ya mwaka 2010 kwamba hata ujenzi huo ni miongoni mwa mambo yaliyomo katika ilani hiyo kwamba suala la ujenzi wa vituo vya polisi pia limepewa
kipaumbele

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga  Hamis Mgeja akiwashukuru watu wote waliochangia katika harambee ya ujenzi wa kituo hicho ambapo lengo lilikuwa ni kukamilisha pesa iliyopelea  kiasi cha shilingi 8,351,500/= na kukamilisha milioni 11,laki 9,na elfu 10 huku wananchi wakicwa tayari wamechangia zaidi ya milioni tatu,na katika harambee hiyo zimekusanywa milioni 9,laki 2 na elfu 2.Na katika pesa hizo chama cha mapinduzi kimechangia mifuko 20 ya saruji,na Mgeja na marafiki zake amechangia milioni 5,laki nane na elfu 30

Ni baada ya harambee ya ujenzi wa kituo cha polisi Didia kukamilika,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Hamis Mgeja akikabidhi shilingi laki moja na nusu kwa kocha wa TIMU YA DIDIA STARS, bwana Sato Bugehu baada ya wajumbe wa kikao hicho kilichofanyika Didia kuchangia pesa kwa ajili ya kuiwezesha timu hiyo,na kama mzawa wa eneo hilo mheshimiwa Mgeja alichangia elfu hamsini papo hapo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم