Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA ABIRIA 40 WA BASI LA ABOOD WANUSURIKA KIFO, BASI LATEKETEA KWA MOTO KAHAMA

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Zaidi ya abiria 40 wamenusurika kifo baada ya basi la abiria mali ya Kampuni ya Usafirishaji ya Abood kuteketea kwa moto katika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

Basi hilo lenye namba za usajili T 285 EAV, lilikuwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kagera lilipokumbwa na tukio hilo la moto leo, Novemba 13, 2026, majira ya saa 11 alfajiri.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Kahama, ASF Stanley Luhwago, amesema kikosi cha zimamoto kilipata taarifa na kufika eneo la tukio, ambapo kilifanikiwa kuudhibiti na kuuzima moto huo.

Kutokana na tukio hilo, abiria wote waliokuwamo ndani ya basi hilo wameelezwa kunusurika, huku basi hilo likiteketea kwa moto.

Chanzo cha moto huo na thamani ya mali iliyopotea bado havijaelezwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com