Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE KILINDI,KITETO WAENDELEZA UJIRANI MWEMA MIRADI YA MAENDELEO






Katika kuonesha ujirani mwema Mbunge wa Kiteto Edward Ole Lekaita na Mbunge wa Kilindi Salehe Mhando wameamua kushirikiana kuhakikisha barabara ya Lengatei- Songe inatengenezwa kwa kiwango cha changarawe na kupitika kwa mwaka mzima.


Mbali ya kushirikiana kusimamia Ujenzi wa barabara hiyo pia Wabunge hao wameshiriki shughuli ya uzinduzi wa shule ya awali na msingi Kijiji cha Lesiot Kata ya Lengatei Kiteto.






Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com