Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

STAMICO YASHIRIKI MAADHIMISHO SIKU YA WAFANYAKAZI 2026


Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wameungana  na wafanyakaz wengine  duniani kote kuadhimisha  Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambapo maadhimisho haya kitaifa  yamefanyika  katika viwanja vya Lunyanywi, Halmashauri ya Mji wa Njombe.

Maadhimisho haya yalikuwa na kauli mbiu ya "Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara Kwa Maendeleo Endelevu Katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050"

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Rasilimali  Watu Mwandamizi wa STAMICO, Bi Leah Jericko  amesema ushiriki wa STAMICO  kitaifa na kwenye Mikoa ni ishara ya kuthamini mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya taifa pamoja na kutambua nafasi zao katika kukuza sekta ya madini nchini.

Aidha, amelishukuru Shirika kwa kuwawezesha wafanyakazi kushiriki katika maadhimisho hayo kitaifa na kwenye Mikoa Mbalimbali na ametoa  wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uzalendo ili kuhakikisha STAMICO inafikia malengo iliyojiwekea.

Kwa upande wake, mfanyakazi Hodari wa STAMICO, mwaka huu wa 2026, Bwn Mark Magessa ameushukuru Uongozi na Watumishi wenzake kwa kumuona anafaa kupata tuzo hiiyo na  amesema kuhudhuria Maadhimisho haya kumewapa fursa ya kujifunza mambo mbalimbali, kubadilishana uzoefu na kujenga mshikamano na  wafanyakazi kutoka taasisi nyingine.

Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani hufanyika kila mwaka Mei Mosi kwa lengo la kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

STAMICO imeshiriki  Maadhimisho hayo kitaifa  Mkoani Njombe sambamba na ofisi  zake zote katika  mikoa ya Dar es Salam, Dodoma, Singida, Geita na Songwe.







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com