Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KWA NINI PICHA ZA UONGO ZILITUMIKA NA KULAZIMISHA DUNIA KUAMINI NI ZA KWELI?

 

Kumekuwepo na juhudi za makusudi za kupinga Ripoti ya Tume ya Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Othman Chande, iliyochunguza mtafaruku uliozuka Oktoba 29 ;lakini wapinzani hao wanashindwa kuleta hoja yoyote ya kisayansi kuzidi uchunguzi wa kina wa siku 150 uliothibitisha kuwepo kwa upotoshaji wa kimkakati uliolenga kuichafua nchi kimataifa.

Ni jambo la kusikitisha na lenye kuleta athari mbaya sana kwa taswira ya Taifa kuona jinsi teknolojia inavyotumika kuipaka matope Tanzania kwa makusudi. 

Tume imebaini kuwa matumizi ya akili mnemba (AI) hayakuwa ya bahati mbaya bali ulikuwa mkakati wa kutengeneza picha za uongo ili kuuchafua uchaguzi wa 2025 na kuaminisha dunia kuwa kuna mauaji ya halaiki. 

Picha ya miili kwenye mifuko ya bluu imethibitika kuwa ya miaka mingi na imetumika katika matukio mbalimbali duniani kabla hata ya Oktoba 2025, jambo ambalo ni uhalifu wa kisayansi unaolenga kuvuruga usalama na diplomasia ya nchi yetu.

Athari za upotoshaji huu ni kubwa kwani zimesababisha taharuki kwa wawekezaji na watalii, jambo ambalo ni hujuma ya wazi ya kiuchumi dhidi ya watanzania. Picha hizo zililenga kuamsha hasira miongoni mwa wananchi na kuchochea mapigano ya ndani ambayo yangeweza kulipeleka Taifa kwenye machafuko yasiyorekebishika, huku zikivunja imani ya umma kwa mamlaka halali za nchi kupitia uongo wa kidijitali.

Ni lazima sasa hatua za kisheria zichukue mkondo wake kwa sababu watu waliotumia picha hizi kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kimataifa hawawezi kuachwa waendelee kuudanganya ulimwengu bila kufikishwa kwenye mkono wa sheria. 

Wale wote waliopiga kelele kupinga ripoti hii wanajua fika kuwa uchunguzi wa jinai ukikamilika hakuna atakayepona kwani utekelezaji wa hatua za uwajibikaji utawagusa wote waliosababisha, waliofadhili na waliotekeleza vurugu hizo.

Dunia imeona nini kilichofanywa na Mange Kimambi, Maria Sarungi, Heche, Tundu Lissu, Mwaipaya, Bongo Zozo, Hilda Newton, na Sativa. Hawa wamekuwa wasambazaji wakubwa wa picha hizo zilizoambatana na maneno na sauti zao. Tume imesema kuhusu haja ya uchunguzi wa jinai na kufikisha watuhumiwa mahakamani,a na ni hawa tena wanapinga ripoti ya Jaji Chande.

Uchochezi wa vurugu na upotoshaji kwa kutumia teknolojia upo wazi na hakika wahusika wanastahili kuwajibika kwa jinai ya kusababisha taharuki nchini. 

Hata chombo cha habari kama CNN na mwandishi Larry Madowo wanastahilki kujipanga kuieleza dunia kwa nini walitumia picha za uongo kuiaminisha dunia kuwa ni za kweli wakati wakijua fika kuwa wanafanya uhalifu dhidi ya ukweli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com