
Victory Senge enzi za uhai wake
Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Victory Emmanuel Senge, amefariki dunia leo Jumamosi, Mei 2, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, kufuatia changamoto za uzazi.Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Jacob Twange.
Victory Senge alikuwa akihudumu kama Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja katika Ofisi ya Mkoa wa Shinyanga.
Mbali na kazi yake serikalini, pia alikuwa mfanyabiashara na mmiliki wa maduka ya nguo ya Victorious yaliyopo Ngokolo Mjini Shinyanga.
Kifo chake kimeacha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzake na wananchi wa Shinyanga waliomfahamu.
Msiba upo Bushushu ya Mwalugoye Mjini Shinyanga.
Mazishi ya mwili wa marehemu Vicky yatafanyika siku ya Jumatano Mei 6 ,2026 Mjini Shinyanga.
R.I.P Vicky







Social Plugin