Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BILA AMANI JUHUDI ZETU HAZIWEZI KUFANIKIWA- MABULA



Na mwandishi wetu, Dar

Amani katika jamii na Taifa kwa ujumla imetajwa kama msingi mkuu wa maendeleo na uhuru katika jamii yoyote, ikielezwa kuwa bila amani, juhudi za kujenga uchumi na kuimarisha uhuru wa mtu binafsi haziwezi kufanikiwa kwa sababu mazingira yanakuwa na hofu na migogoro na kutopatikana muda na uhuru wa kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aidha katika hali ya amani, watu wanaweza kutumia haki zao za kikatiba, kutoa maoni, na kushiriki katika ujenzi wa taifa kwa hiari huku pia amani ikitajwa kama kiungo muhimu katika kuendeleza umoja wa kitaifa, ambao ni nguzo muhimu inayowezesha jamii kusonga mbele kwa pamoja kuelekea malengo ya kimaendeleo.

"Amani ni ushirikiano, bila amani hakuna kitakachofanyika na hata ushirikiano unaotusaidia kutengeneza mia mbili, mia tatu za kila siku hautakuwepo tena kama amani itatoweka." Amesema Bw. Ibrahim Mabula, Mkazi wa Ilala Dar Es Salaam, wakati akizungumza na Mwandishi wetu leo Aprili 14, 2026.

Katika maelezo yake, Bw. Mabula amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulinda na kuitunza amani iliyopo nchini, akimuombea kwa Mwenyenzi Mungu aendelee kumpa maono zaidi katika kuhakikisha tunu muhimu za Taifa zinaendelea kudumishwa kwa ustawi na maendeleo ya Taifa.

Kwa upande mwingine Bw. Said Makele, Mkazi wa Ilala amewataka watanzania kujifunza kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025 na namna ambavyo uhuru ulikosekana katika baadhi ya maeneo kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa muda wote kama ilivyokuwa awali pamoja na hofu iliyokuwepo, akimuhamasisha kila mmoja kushiriki kueneza amani na kutoa elimu ya umuhimu wa amani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com